TIRDO WA WAKO SABASABA WANA MAMBO MAZURI WATEMBELEE
DAR ES SALAAM
SHIRIKA la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) wamewataka wananchi kutembelea Banda lao katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara(SABASABA) yanaoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam .
Hayo yamebainishwa leo Julai 3,2023 na Mtaalam wa Nishati ,Ali Moh'd Rashid wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kwamba wamekuja na tafiti mbali mojawapo ni utaalam juu ya matumizi bora ya nishati .
Amesema kuwa matumizi bora ya nishati ni kutumia nishati kwa namna ambayo inapunguza upotevu wa nishati na kufikia matokeo sawa na bora bila kuathiri utendaji.
Aidha ,ameeleza kwamba inapaswa kufanya ukaguzi wa mifumo ya nishati Kila baada ya muda ili kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.
Pia,amesema kwamba kutumia vifaa vinavyotumia teknolojia za kisasa ambazo zinatumia nishati kwa ufanisi mfano Taa za LED.
Sanjarari na hayo, Mtaalamu Rashid ameendelea kwa kusema kwamba matumizi ya vyanzo vya nishati mbadala ikiwemo jua,upepo kwa kupunguza gharama.
"Kupunguza matumizi ya nishati,biashara na mashirika yanaweza kupunguza bili zao za nishati na gharama za uendeshaji",alisema
Amebainisha pia maeneo ya upotevu wa nishati na kutoa mapendekezo ya kuboresha kunaweza kusababisha uokoaji mkubwa wa nishati.
Aliendelea kwamba kuboresha utendaji wa vifaa kwa kufanya ukaguzi kutasidia kutambua mahitaji ya matengenezo na kuboresha utendaji kazi wa kifaa.
Alimalizia kwamba kuna faida kwa mzalishaji wa nishati mfano Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) huduma ya nishati inaweza kuwafikia watumiaji wengi kuwa na matumizi bora ya nishati
Post a Comment