Ads

MKUU WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE ATEMBELEA SABASABA

 


MKUU wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA) ,Prof.Haruni Mapesa ametembele Banda la Chuo katika Maonesho ya 49 Kimataifa ya Biashara(SABASABA) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius K.Nyerere  Jijini Dar es Salaam.


Prof.Mapesa ametembelea Leo Julai 3,2025 na pia ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha  watanzania kujitokeza kwa wingi kutembelea Banda lao  ili kupata historia ya chuo na kujionea bunifu mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi.


Aidha ,amesema Chuo cha MNMA kinahistoria ndefu kilianzishwa na Mwalimu Nyerere mwezi Julai 29, 1961 miezi michache kabla yakupata uhuru.


Pia ameeleza kwamba Chuo kilianzishwa kwa lengo la kuandaa viongozi wa Tanzania ambao wameongoza baada yakupata uhuru.


"Chuo hiki kimepewa jina la Mwalimu Nyerere  kwa ajili ya kumuenzi mwalimu kwa juhudi kubwa yakuwaelimisha watanzania lakini pia kuokoa nchi ya Tanzania",alisema


Hata hivyo, amesema kuwa Chuo kina majukumu matatu makubwa yakutoa elimu yaani mafunzo kwa wataalam kwa kuanzia ngazi ya  wataalamu wa cheti hadi shahada za Umahiri.


Sanjari na hayo Prof.Mapesa amesema kwamba Chuo kina jukumu lakufanya utafiti na kutoa machapisho mbalimbali yanayohusu utafiti huo.


Profesa Mapesa pia amewakaribisha vijana wanaojiandaa kujiunga na chuo kutembelea Banda Hilo kwani wataweza kupata nafasi yakujiandikisha  hapo hapo na kupewa usajili.


Aliendelea kwamba hiki ni chuo kinachotunza historia ya nchi  na wao wamejipanga vizuri kuwaelimisha watanzania kwa weledi.

No comments