Ads

TAKWIMU ZA WATALII WALIVYO CHANGAMKIA VIVUTIO VYA WANYAMA NCHINI ZINASHANGAZA

 


Afisa Muhifadhi  mkuu  wa MAMLAKA ya Wanyamapori Tanzania(TAWA)   TAWA, Dkt. Gladstone Mlay ameeleza kwamba TAWA imekusanya shilingi  bilioni 3.9 kupitia vivutio vyake vya utalii ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kukuza Pato la Taifa.

Dkt Mlay amebainisha hayo Leo Julai 3,2025 na Afisa Muhifadhi TAWA, Dkt. Gladstone Mlay wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la TAWA  na kufafanua kuwa   kwa mwaka 2024 jumla ya watalii Milioni 5.3 wametembea hifadhi za Taifa ambapo watalii wa ndani milioni 3.2 na watilii  wa Kimataifa milioni 2.1 wamepita katika maeneo mbalimbali yanayosimamiwa na Mamlaka hiyo.

Pia amesema watalii wanapotembelea kwa wingi wanatoa fursa kwa wananchi kwa kuuza bidhaa mbalimbali katika maeneo yanayozungukwa na hifadhi hivyo jamii inanufaika.

‎Amesema  kwamba wananchi tuendelee kutunza hifadhi zetu na maliasili ni za kwetu sote ili tuweze kupata fedha kwa ajili ya kuongeza ama kukuza uchumi ya nchi yetu.

Kwa upande wake, Afisa Habari TAWA ‎,Beatus Maganja amesema kwamba Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa watanzania wote na wawekezaji kuwekeza .

 Amesema kwamba wananchi watumie fursa ya maonesho kwenda kutembele na kujionea wanyama pori ambao wapo kabla ya kilele.

"Njooni watanzania kujionea wanyama kwani baadhi wanawaona wanyama katika kupitia luninga na kwenye mitandao ya kijamii lakini Leo hii ni fursa kuwaona wanyama pori kwa ukaribu zaidi na kwa uhuru",alisema Maganja

Hata hivyo amesema katika maonesho haya ni fursa mojawapo kwa wananchi kwani unaweza kuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na tabia za wanyama wakali na waharibifu kwa mfano fisi madoa unaweza kujifinza tabia zao na kujua namna gani yakuweza kuepuka hawa wanyama katika maeneo mbalimbali waliokokua wakisumbua.


No comments