Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya
Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (PCC) Dkt. Ladislaus Chang’a
akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 22, 2025 jijini Dar
es Salaam katika warsha ya kuwajengea uwezo kuhusu utabiri wa msimu wa mvua za
masika 2025.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka
wanahabari nchini kuzingatia miongozo ya utoaji wa taarifa za hali ya hewa pamoja
na kuongeza ubunifu na ufanisi katika
kuandaa taarifa hizo kwa kushirikiana na wataalamu ili kuhakikisha wananchi
wanapata taarifa sahihi kwa wakati.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 22,
2025 jijini Dar es Salaam katika warsha ya kuwajengea uwezo kuhusu utabiri wa
msimu wa mvua za masika 2025, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya
Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (PCC) Dkt. Ladislaus Chang’a, amesema
kuwa wanahabari wanapaswa kutoa taarifa sahihi ili kufikia malengo na kuleta
tija kwa Taifa.
“Tuendelee
kuelimisha jamii, kuwa na uthubutu, ubunifu katika utekelezaji wa majukumu yenu
ya kufikisha taarifa, kufanya hivyo mnasaidia kuokoa maisha ya watu kwa kuepukana na athari za mabadiliko ya hali ya
hewa ” amesema Dkt. Chang’a
Katika hatua nyengine ameeleza kuwa mwaka 2024 kulikuwa
na ongezeko la joto duniani 1.55 na kuvunja rekodi, huku nchini Tanzania
takwimu zinaonesha kulikuwa na ongezeko la joto 0.7.
“Kila mwaka joto linaendelea kuongezeka hali ambayo inatokana
na changamao ya uwepo wa hali ya mbaya ya hali ya hewa ikiwemo uwepo wa
vimbunga” amesema Dkt. Chang’a.
Dkt. Chang’a ameishukuru Serikai ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya hali ya hewa, kwani
mwaka 2024 walifanikiwa kununua rada mbili ambazo zimefungwa Mkoa wa Kigoma na
Mbeya na kuifanya Tanzania kuwa Nchi pekee Afrika ya Mashariki katika kuwa na vifaa
bora vya hali ya hewa.
Meneja wa Ofisi Kuu ya Utabiri TMA Dkt. Mafuru Kantamla, amesisitiza umuhimu kwa
wanahabari kufanya kazi kwa kuzingatia uweledi, maadili pamoja na kuendelea
kuwa na nidhamu katika kuhabarisha jamii kuhusu taarifa za hali ya hewa.
Nao wanahabari wameishukuru TMA kwa kuendelea
kuwajengea uwezo wa kuandaa taarifa za hali ya hewa ambazo zimeweza kuisaidia
jamii na wadau mbalimbali kujitayarisha na mabadiliko ya hali ya hewa.
Mwandishi wa habari wa Kiss Fm Bw. Mussa Khalid,
amesema kuwa taarifa za hali ya hewa zimekuwa na manufaa makubwa kwa jamii hasa
katika kuzuia majanga na kusaidia kutekeleza mipango ya serikali..’’Wanahabari
tunatambua juhudi za TMA katika kuboresha ushirikiano na utoaji wa taarifa za
kisayansi kwa umma”.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment