AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAWAZAWADIA WASHINDI WA KAMPENI YA TWENDE KIDIGITAL TUKUVUSHE JANUARI
Na Mwandishi wetu-Dar es salaam
Akiba Commercial Bank imewashukuru wateja wake kwa kushiriki katika kampeni "twende kidigital tukuvushe Januari" na imewahimiza kuendelea kutumia huduma zake za kidijitali kama vile ACB Mobile, Internet Banking, ACB VISA Card, na ACB Wakala ili kufurahia uzoefu wa kipekee wa kibenki.
Wateja walionyesha furaha na shukrani kwa Akiba Commercial Bank kwa jitihada zake za kuimarisha huduma za kidijitali ambazo zimeboresha uzoefu wao wa kibenki kwa kuwapatia urahisi na wepesi wa kupata huduma za kifedha wakiwa mahali popote na wakati wowote
Miongoni mwa wateja akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa zawadi hizo, Bw. Alfayo Zephania alieleza jinsi alivyopokea furaha habari njema za kuibuka mshindi wa kampeni hiyo amesema "Nilifurahishwa sana na tarifa ya ushindi wangu na ninaishukuru Benki ya Akiba kwa kujali wateja wake na kutoa huduma bora na anatoa rai kwa watu wengine kujiunga na Akiba Commercial bank wanufaike na mengi ikiwemo mikopo ambayo imenivusha pakuwa katika biashara zangu”
Naye Mteja Ezekiel Willium alielezea furaha yake kwa zawadi aliyoshinda, akisema kuwa ushindi huo umempa hamasa zaidi ya kushiriki kwa bidii ili kupata zawadi kubwa zaidi katika droo kuu ya mwisho wa kampeni.
Aidha Akiba Commercial benki imewashukuru wateja wake kwa kushiriki katika kampeni hiyo na inawasihi waendelee kutumia huduma za kidijitali za benki .
Post a Comment