Ads

RAIS SAMIA ALITAKA JESHI LA POLISI KUWA MACHO WAKATI KABLA NA BAADA YA UCHAGUZI

 


 

Rais Samia Suluhu Hassan amesema inashangaza kuona jinsi kifo cha mmoja wa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mzee Ali Kibao kilichotokea hivi karibuni kuibua wimbi kubwa la kulaumu, na kusema kuwa hali hiyo si sawa.


Rais Samia ameyasema hayo mkoani Kilimanjaro wakati akihitimisha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi pamoja na kufunga mkutano wa Maofisa Waandamizi ya Jeshi hilo leo Septemba 17, 2024.
Aidha Rais Samia amezionya balozi za nchi mbalimbali zinazotoa matamko na kuielekeza serikali nini cha kufanya kufuatia matukio ya mauaji na utekaji yanayotokea hapa nchini.


"Kumepangwa Sjui kushushwa Moto mpaka Samia aseme 'basi nime-surrender naondoka' hiyo ni Serikali ya Samaki lakini Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiondoshwi hivyo."
“R4 si sababu ya utovu wa nidhamu, si sababu ya kukiuka sheria za nchi sheria za nchi zipo pale pale, ni vizuri wasisahau mapito waliyopita.
Serikali imejitahidi sana kurejesha uhuru wa vyama vya siasa,uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa raia.
“Kwa ujumla wale waliokuwa uhamishoni walirejea nchini, waliokuwa na kesi za jinai na wengine tulizifumbia macho, waliokuwa jela tuliwatoa sasa wapo huru na wanaendelea na shughuli zao ikiwamo shughuli za kisisasa, lengo letu likiwa kuwaleta watu pamoja ili tuweze kujenga nchi yetu.
“Sasa watu wale wale wanaposahau yote hayo na wanapofanya vitendo vya kutoa kauli zinazoharibu au kuturudisha nyuma sisi hatutokuwa tayari kuwaruhusu kufanya hivyo. ''


Amani ya nchi yetu tatailinda kwa gharama yoyote ile,” amesema Rais Samia .


“Katika kipindi cha uchaguzi kila mmoja wetu anatakiwa kujipanga kufanya kazi zake vizuri zaidi tumejipambanua kulileta Taifa letu pamoja, hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha Taifa letu linabaki kuwa moja na salama, uchaguzi utapita lakini Tanzania itabaki, tunataka kubaki na Tanzania iliyo salama na Tanzania yenye utulivu ili shughuli za maendeleo ziweze kuendelea.


“Nalitaka Jeshi la Polisi kuwa macho katika kipindi chote cha kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
 Polisi ihakikishe yeyote anayejaribu kuhatarisha amani ya nchi yetu kwa kisingizio za chaguzi hizo anachukuliwa hatua haraka na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” amesema Rais Samia

No comments