KKKT YAKEMEA MAUAJI NA UTEKAJI NCHINI ,WAKIMZIKA ASKOFU SENDORO
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dk Alex Malasusa ametumia ibada ya maziko ya aliyekuwa Askofu wa Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa hilo, Chediel Sendoro kukemea matukio ya utekaji na mauaji yanayoendelea nchini na kuiomba Serikali kuruhusu meza ya majadiliano.
Dk Malasusa amezungumza hayo leo Septemba 17, 2024 wakati akitoa salamu za kanisa katika ibada hiyo, iliyofanyika katika Kanisa Kuu Mwanga, mkoani Kilimanjaro, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali akiwemo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko.
Askofu Sendoro alifariki dunia Septemba 9, 2024 kwa ajali iliyotokea katika eneo la Kisangiro, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro saa 1:30 usiku, baada ya gari alilokuwa akiendesha aina ya Toyota Prado, akitokea Kileo kuelekea nyumbani Mwanga, kugongana uso kwa uso na lori.
Akitoa salamu za Serikali, Dk Biteko amesema suala la utekaji na mauaji yanayoendelea nchini, tayari Rais Samia Suluhu Hassan alishatoa maelekezo ya uchunguzi kufanyika kwa haraka.
Post a Comment