Zaidi ya wafugaji 3,000 kutana kujadili changamoto zao.
Zaidi ya wafugaji 3,000 na wadau wengine wa sekta ya mifugo kutoka maeneo mbalimbali nchini, wanatarajia kukusanyika wilayani Igunga mkoani Tabora kwa ajili ya kufanya kongamano kubwa linalolenga kujadili mafanikio na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Hayo yameelezwa leo mjini Igunga na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT), Ally Manonga.
Manonga amesema licha ya serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kutatua matatizo mengi yaliyokuwa yanaikabili sekta ya ufugaji nchini, bado zipo changamoto chache za kufanyia kazi.
"Changamoto nyingi za wafugaji zimetatuliwa na zinaendelea kutatuliwa lakini bado kuna masuala ambayo pia yanatakiwa kutupiwa jicho ili kuyapatia ufumbuzi wa kudumu," amesema bila kuyataja.
Manonga amesema kuwa kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika keshokutwa Julai 28, 2024 litajadili mafanikio, changamoto na kupendekeza namna ya kutatua changamoto hizo.
Post a Comment