Ads

VETA YAPATA MWAROBAINI WA USIKIVU HAFIFU ,KUPIGWA PESA SASA BASI




 Mwamba wa habari

Imeelezwa kuwa Kubuniwa kwa kifaa cha usikivu  hapa nchini huenda watu wenye changamoto ya usikivu wakapata mkombozi atakaye wasaidia katika changamoto hiyo.

Akizungumza na Mwamba wa habari  leo Julai 1-2024 katika banda la VETA katika maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa  mbunifu wa kifaa hicho mwalimu Innocent Maziku, amesema changamoto ya usikivu aliyokuwa akipambana nayo ndiyo ilimsukuma kutafuta suluhisho lake.

Maziku ambaye ni Mwalimu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta)  Kigoma amesema  kifaa hicho kinauwezo wa  kuwasaidia watu wenye changamoto ya usikivu hafifi na wakasikia  vizuri.

Ameeleza kuwa huenda kubuniwa kwa kifaa hicho  kutashusha gharama za ununuzi ambazo watu wenye changamoto hiyo walikuwa wakizipata katika kununua vifaa kutoka Shilingi  500,000 kwa kifaa cha sikio moja cha analogia na Shilingi milioni 1.2  kwa kifaa cha kidigiti.

Akielezea kwa hisia na furaha aliyo nayo baada ya kuona mafanikio makubwa ya chombo hicho Maziku amesema .

“Nilipata changamoto hii ghafla alipokuwa darasa la sita, ikanifanya kupata shida  shuleni masomoni  na kifaa nicho nunuliwa kilishindwa kuni Saidia’’ Amesema

 

No comments