Ads

DKT MPANGO KUWA MGENI RASMI KONGAMANO LA WACHUMI TANZANIA


Na Francisco Peter, Dar es salaam.

Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika Kongamano la mwaka la Jumuiya ya Wachumi Tanzania (EST) litakalofanyija Julay 12/2024 katika ukumbi wa Bank kuu ya Tanzania (BOT) Dar es salaam.

Madhumuninya kimsingi ya EST ni kukuza taaluma katika uwanja wa uchumi,utafiti wa kiuchumi,mipango Ya kuichumi,majukwaa ya mabadiliano juu ya mada za kiuchumi na zinazohusiana,na sera ya uchumi kwa.kuleta wanachama na washirika wa taaluma ya uchumi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Mjumbe wa Baraza La Uongozi wa Jumuiya ya Wachumi Tanzania (Governing Council Member) Geoffrey Mwambe Amesema mkutano huo unaangazia tafakari muhimu ya mwelekeo wa uchumi kimataifa kuwezesha michakato ya kufanya maamuzi kwa watunga sera kwa uchumi wa taifa shirikishi na endelevu.

Mkutano huo utawaleta pamoja wataalamu na watendaji ,ni fursa ya kukuza ubadilishanaji wa ujuzi wa ushirikiano,na kubadilishana uzoefu huwapa wataalamu na watendaji fursa ya kuimarisha ulizini wao,ujuzi,na kujifunza mikakati ya kujumuisha mitindo ya hivi punde ya kiuchumi, hivyo ametoa wito kwa wanachama kujiandikisha na kuhudhuria pamoja na wafadhili kufadhili shughuli zinazofanywa na EST.

"Tunao wachumi katika maeneo mbalimbali nchini,wapo TRA,wapo kwenye halmashauri pia uchumi umegawanyika katika maeneo mbalimbali kuna uchumi wa afya,elimu,jamii nk". Amesema Mwambe 

Aidha ametaja Malengo Makuu ya mkutano huwa kuwa ni kupata majawabu katika changamoto zilizopo katika jamii,"haitakuwa na maana wachumi tupo alafu tunafanya mambo bila kuzingatia ushauri wakitaalamu".

Pia mwambe amesema katika mkutano na kongamano hilo wanatarajia kuhudhuliwa na Watu 300-500 ambapo wamealika wazungumzaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Sambamba na hayo wamenawaalika vyama vyote vya kitaaluma ikiwa ni pamoja na Bodi ya manununizi,wahasibu,bodi za wakandarasi,bodi ya mainjinia,bodi ya biashara,chama cha wanasheria,sekta za umma karibu 267, sekta binafsi,cti,tccaa,umoja wa bank Tanzania na Taasisi zingine pia wanakaribisha mtu mmoja mmoja.

Pia Wamewataka wachumi wote kushiriki katika kongamano hilo kwa kujisajili kupitia www.wachumi.com ambapo watakutana na link ya kujisajili kushiriki kongamano hilo.

Kaulimbiu ya mwaka huu ni Majukumu ya Jumuiya ya wachumi Tanzania katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.

No comments