Ads

SHAMTE : WANAHABARI KALAMA ZENU KUSISITIZA SHERIA MPYA ZA HABARI MJUMBE WA BODI TAMWA.

Na, Thuwaiba Habibu, Zanzibar 

Mjumbe wa Bodi cha Cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA) Hawra Shamte aliwataka waandishi kuendelea kutumia kalamu zao kuhakikisha sheria ya habari rafiki zinapatikana.

Ameyasema hayo katika kikao cha kutoa mrejesho wa kazi za mapitio ya sheria ya habari zenye vifungu vinavyo kinza uhuru wa habari zilizofanywa kwa mwaka mzima ambacho kimefanyika Tamwa Tunguu Unguja alisema tunategemea sheria zetu zitatoka kwa makatibu wakuu na kuacha kupigwa dana dana kutokana na ahadi tunazopewa kwa sheria zetu kuu mbili za habari ikiwa ni wakala wa usajili magazeti, na tume ya utangazaji kwa sababu tushazisemea sana na tunazidi kuziandikia hadi tuone mafanikio.



Pia alisema kuna vyombo vya habari hawataki kusikia habari kuhusu sheria hizo lakini ipo haja ya kutumia vyombo vyengine ili kuweza kufikia lengo letu la kupata sheria mpya.

Kwa upande wake Afisa mratibu wa sheria za habari Zaina Mzee alisema tunaenda mwaka wapili katika kuhamasisha upatikanaji wa sheria mpya ya habari na tumefakiwa kwa kiasi kikubwa licha ya kuwa hatuja ipata sheria rafiki.

Tulishakutana na viongozi mbali mbali kujali jambo hili kwa jumla ya mikutano mitano ambayo ilifanywa na wadau wa habari (zameco) wakiwa na tume ya marekebisho ya sheria ,tume ya utangazi viongozi wa baraza la wawakilishi na viongozi wengine kujadili suala sheria za habari ambalo bado halija pata muwafaka.

Pia alisema tumeandaa mafunzo kwa waandishi wa habari kwa unguja na pemba lengo la kufanya kuhamishaji kuhusu sheria za habari na tulifanikisha hilo.

Waandishi waliopata mafunzo waliyafanyia kazi kwa kufika mpaka kwa wanasheria kutaka wapate ufafanuzi wa sheria na pia walipata nafasi ya kuwaelimisha wengine juu ya umuhimu wa kuwa na sheria za habari mpya.

Aidha alisema sheria ya habari iliyo rafiki pekee ndio inayoweza kuiheshimisha tasnia ya habari hivyo wadau wa habari wanapambana kuona inajitengemea na haingiliwi na mamlaka yoyote kwani kufanya hivyo kunakosesha uhuru wa kujieleza na kutoa taarifa.

Akiwasilisha mrejesho wa kazi kwa niaba ya afisa mfatiliaji na tathimini khairat Haji alieleza tumewapatia nafunzo waandishi 25 kutoka unguja na pemba ambao walifanikisha kuandika story 161 ambazo ziliwasilizwa katika vyombo tofauti ikiwemo radio, Tv,mitandao ya kijamii na magazeti Lengo ni kufanya uhamasishaji wa kupatiwa sheria mpya.

Wanahabari 25 waliopatiwa mafunzo 15 ni kutoka unguja na 10 ni pemba ambao walitumia elimu hiyo kuhakikisha taarifa walizotoa zinaelimisha umma juu ya kitu wanachokitaka.

Alieleza kuwa mrejesho unaonesha waandishi 15 kutoka unguja walipatiwa elimu hiyo 10 tu ndio walifanikiwa kutoa mrejesho wa kazi walizofanya ambazo ziliweza kuzua maoni tofauti katika vichwa vya watu.

Alisema katika hao 10 walitoa mrejesho wa kazi redio zilikuwa 2, television 4, magazeti 2 na mitandao ya kijamii 2 ambapo Tv ilitowa kazi 7 sawa aslimia 19% magazeti 5 kwa 16% mitandao ya kijamii 6 sawa16 % na radio 19 kwa 51%.

Kwa upande wake muandishi mkongwe salim said salim aliwaomba waandishi kutokata tamaa na kuendelea kuandika na kusemezea sheria hizo mpaka kufikia malengo.

Pia alisema tunatakiwa kuandikia story/au makala zitakazo onesha mifano ya nchi waliofanikiwa kuwa na sheria a habari rafiki kama kenya na uganda ili kuleta hamasa zaidi ya kupatiwa sheria mpya.

Nao mwaandishi waliopatiwa mafunzo hayo Asia mwalim na Amrat kombo walisema tuendelee kuandika kwasababu lengo halija timia na sisi ndio wahanga tukipata sheria rafiki itakuwa rahisi kwetu kuweza kupata taarifa bila vikwazo.

No comments