Ads

MRAMBA :SERIKALI ITAENDELEA KUIWEZESHA EWURA ILI KUONGEZA UFANISI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesema Wizara hiyo itaendelea kuiwezesha Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati (EWURA) ili iweze kutekeleza majukumu yake katika mazingira yanayokubalika ndani ya Sekta hiyo.

Mhandisi Mramba ameyabainisha hayo alipotembelea katika Banda la EWURA katika Maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam.

Amesema EWURA imekuwa ikifanya kazi nzuri ya kudhibiti huduma za maji na nishati.

"Naipongeza EWURA Kwa nzuri ya kudhibiti huduma za maji na nishati 

Kama mnavyoona huduma zinazodhibitiwa na EWURA zinapatikana na wameweza kudhibiti upatikanaji wa huduma na bei huduma inayotolewa pamoja na ubora wa huduma hiyo."amesema Mhandisi Mramba 

Katika eneo la nishati Mhandisi Mramba amesema EWURA wamekuwa wanadhibiti eneo la umeme na huduma za gesi asilia pamoja na mafuta.

"Katika eneo la bei mnafahamu kwamba nchi yetu ni miongoni mwa nchi zenye bei ya chini sana ya huduma za umeme nchi yetu ni nchi yenye bei ndogo za umeme ukilinganisha na majirani zetu wa karibu"amesema Na kuongeza kuwa 

"Kwa siku za karibuni nyingi ni mashahidi kuwa ubora wa huduma za umeme umeimalika sana kule kukatika sana Kwa umeme yaani mgao wa umeme umepungua Kwa kiasi kikubwa.

Amesema ubora huo umefikia Mahali ambapo hakuna shida ya umeme huku ukiwa katika kiwango cha kuridhisha na kueleza kuwa Serikali itaendelea kuboresha hivyo ni wajibu wa EWURA kudhibiti na kusimamia.

Kwa upande wa eneo la gesi asilia EWURA amesema EWURA imesaidia sana huku ikiendelea kufatilia pamoja na kutoa leseni kwa wale wanaojenga vituo vya gesi asilia na vituo vya mafuta .

Vilevile amesema katika eneo la mafuta EWURA imekuwa ikisimamia a huduma zinazotolewa katika vituo hivyo Ili vikizi vigezo vijavyokidhi mahitaji ya jamii .

",Sisi kama Wizara ya nishati wajibu wetu kuhakikisha kwamba EWURA anafanya kazi yake kulingana na Sheria sera na sera zilizopo"amesema Mhandisi Mramba.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dk. James Mwainyekule, amesema mwezi uliopita walisaini mkataba na Tanesco kupima utendaji kazi na namna ya utekelezaji kazi.

"Uwekezaji huu unafanywa na serikali sasa hadi Juni 30, mwaka huu ubora wa mafuta ulifikia asilimia 97. Tunazingati bei katika soko la dunia tukifuatilia na kila mwezi bei zilishuka na kupanda kulingana na soko la dunia.

"Magari takribani 5,000 yanatumia gesi hadi sasa na hii imesaidia kwa asilimia kubwa kupunguza dola kutumika katika kiagiza mafuta nje, kwa sababu gesi hii ya mafuta inatoka nchini."

No comments