PURA: SERIKALI IMEBORESHA MIUNDO MBINU VIWANJA MAONESHO SABASABA.
Na ,John Luhende ,Mwamba wa habari.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Halfani Halfani ameipongeza Serikali kwa kuboresha miundombinu maonesho ya biashara Sabasaba.
Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo leo Julia 11.2024 alipotembelea Banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) katika maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa yanayoendelea Jijini Dar es salaam.
"Miaka ya nyuma ilikuwa kama gulio lazima uje na kofia kujikinga na vumbi lakini mwaka huu hainahaja ya kuvaa kofia Serikali kwa kweli imejitahidi imewekeza Sana "Alisema.
Katika hatua nyingine Halfani amesema PURA imekuwa ikifanya matayarisho ili kivitia wawekezaji.A
idha, imesema mkoani Mtwara imepata mwekezaji mpya wa uchimbaji wa gesi asilia atakayezalisha futi za ujazo milioni 100 kwa siku.
Amesema wanatarajia kiwango hicho kuongezeka na kitasaidia upatikanaji wa gesi ya uhakika.
Vilevile ameeleza kuwa kwa kipindi kirefu wametegemea gesi ya baharini hivyo waamini gesi hiyo itakuwa mpango madhubuti.
Aidha maeneo ya Songosongo Kilwa na Mnazibay Lindi pia wanazalisha futi za ujazo milioni 250 kwa siku na kiasi kikubwa kinatumiwa kuzalisha umeme.
“Asilimia 50 ye gesi hii inazalishia umeme na kiasi kingine minatumika kwenye matumizi mengine,” amesema Halfani.
Kuhusu majukumu ya PURA amesema ni kumshauri Waziri wa Niashati masuala ya mkondo wa juu wa utafutaji, uzalishaji na usambazaji wa gesi nchini.
Amesema jukumu la pili ni kusimamia ufanisi wa juu wa sekta kuhusu utafutaji gesi ili kujua gharama za utafutaji na wapi.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa pia wana jukumu la kuhakikisha Watanzania wanashiriki kwenye jukumu la utafutaji na uzalishaji wa gesi.
Pamoja na hayo amefafanua kuwa PURA pia ina jukumu la kutunga sera ndogo za kuhakikisha utendaji kazi unakuwa wa ufaniisi lakini pia wanasimamia uuzaji wa gesi nje ya nchi
Post a Comment