Ads

PROFESA KUSILUKA ASISITIZA UBORA WA CHUO KIKUU DODOMA

MAKAMU  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Lughano Kusiluka, amewakaribisha Watanzania kwenda kusoma katika chuo hicho kwa sababu programu zote zinazofundishwa vyuo vingine wanazo.


Profesa Kusiluka ameyamebainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam.

Akitaja mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho ni ya madaktari, wauguzi, wataalam wa lishe tiba, afya ya jamii.

"Tunafundisha wataalam katika maeneo mbalimbali kama vile biashara, uchumi, ujasiriamali, masoko na mambo yote yanayohusiana na biashara, lakini biashara katika miaka ya siku hizi ni lazima uwe unajua kuifanya kisomi,” amesema.

Katika hatua nyingine Profesa Kusiluka alitoa wito wajasiariamali na wafanyabiashara wa vyakula wafike katika chuo hicho kwa kuwa wanazo formula za tiba lishe za kukabili magonjwa yasiyoambukiza.

"Watu waje tushirikiane tutengeneze tiba lishe, Tanzania yenye afya ndiyo itakayotupeleka kwenye dira ya maendeleo ya mwaka 2050, tunataka watu wavipate kutoka sehemu mbalimbali,” amesema Profesa Kusiluka.

Aidha amesema Tanzania imejitangaza vizuri na ni nchi inayovutia kwa wawekezaji kutokana na juhudi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema Chuo hicho kinaunga  mkono juhudi hizo za Serikali kwa kuandaa wataalam katika sekta mbalimbali

Aliongeza kuwa wana mpango wa kutafuta wadau na wabia waanze kutengeneza vyakula lishe ambayo ni tiba ili vipatikane kirahisi sokoni. 

No comments