TPDC YAINGIA MAKUBALIANO NA WAWEKEZAJI KUFANYA KATIKA SEKTA YA NISHATI YA NISHATI YA GESI
Na Francisco Peter
SHIRIKA Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) limeingia mkataba wa makubaliano na kampuni mbili za uwekezaji katika nishati ya gesi, Rosetta na Afrika 50 ili kuwezesha kufanya upembuzi yakinifu ya ujenzi na uendelezaji wa mradi wa gesi kimiminika (NLG) na kuisambaza mbali na maeneo ambayo mabomba ya gesi yamepita.
Akizungumza leo Mei 17, 2024 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mussa Makame amesema kwamba mchakato wa ujenzi huo unaweza kuchukua kipindi cha miaka miwili hadi kukamilika kwake.
Kwa sasa nishati ya gesi inapatikana zaidi katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara ambako ndiko mabomba yamefika pia kuna vituo vya ujazaji gesi iliyoshindiliwa (CNG)inayotumika kwenye vyombo vya usafiri na changamoto ambayo ipo ni kuifikisha katika maeneo ya mbali,
Changamoto hiyo inatokana na kukosekana kwa uwekezaji mkubwa wa mabomba ili kuweza kusambaza nishati ya gesi asilia na CNG nchi nzima na kutokana na kushindwa kusambaza miundombinu hiyo katika mikoa ya mbali ndio sababu ilisababisha kuingia mkataba huo na wenzetu hao ili kufanikisha mchakato huo, amesema.
Amesema kuwa kinachokwenda kufanyika ni kupunguza ujazo wa gesi kimiminika ambapo kama ulitakiwa kuweka futi za ujazo moja hivyo utaweka fiti za ujazo 600 jambo linalosaidia kubeba ujazo mkubwa zaidi na kuipeleka mbali zaidi ya pale ulipofanyia uchakataji na kuifanya kuwa kimiminika.
Ameweka wazi kuwa kama hujafanya mchakato na kuamua kuipeleka kwa umbali wa km 400 au 500 bei ya kuiuza huko inaweza kukaribia gharama ya usafirishaji jambo ambali inakuwa ni kufanya kazi ya hasara kitu ambacho hakina tija katika suala hilo.
Amesisitiza kuwa mikoa ambayo itapewa kipaumbele ni ili yenye viwanda, uchimbaji wa madini ukiwemo Morogoro, Tanga, Iringa na Mwanza lengo likiwa kupunguza matumizi ya mafuta mazito na makaa ya mawe.
Naye Paul Makanzi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC, amesema kuwa mradi huo ukikamilika utakwenda kupunguza matumizi ya fedha za kigeni hususan kwa wenye viwanda na wanaoendesha mitambo mikubwa kwa ajili ya kununulia mafuta.
“Huu ni mwanzo mzuri katika kushirikiana na wenzetu ili kufikia malengo na mafanikio tulipewa ili kuyafikia kama shirika na utaweza kuwafikia watu wengi zaidi na utafanikisha jamii kutumia nishati safi hata katika kupikia majumbani,” amesema.
Pia Balozi wa Misri hapa nchini, amesema kuwa mradi huo utafanyika kwa awamu mbili na utafikia dola za marekani milioni 100 na anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kukubali kuingia makubaliano hayo ili kuleta tija.
Kampuni ya Rosetta Energy Solutions ni kampuni tanzu ya kampuni Taqa kutoka nchini Misri na Afrika 50 ni kampuni ya kifedha inayomilikiwa na Serikali za Kiafrika ikiwemo Tanzania na Benki ya Maendeleo Afrika kwa pamoja zitashirikiana katika kuwezesha kufanya upembuzi yakinifu ya ujenzi na uendelezaji wa mradi wa gesi kimiminika (NLG) na kuisambaza mbali na maeneo ambayo mabomba ya gesi yamepita.
Post a Comment