SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA YA SEKTA YA UBUNIFU
Na Francis Peter, Dar es Salaam
Serikali
imesema inaendelea kuboresha mazingira ya sekta ya ubunifu katika nyanja
mbalimbali na kuhakikisha kuwa teknolojia na bidhaa zinazobuniwa na Watanzania
zinaweza kushindana na bidhaa kutoka mataifa mbalimbali Duniani.
Aidha Prof Nyoni amesisitiza kuwa Serikali
imejidhatiti kuhakikisha inawasaidia vijana wabunifu kutengeneza wigo mpana wa
ajira kupitia bunifu zao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na
Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu amewakaribisha wadau na watu mbalimbali
katika wiki ya ubunifu itakayofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Posta Jijini Dar es salaam,(JNICC) ambapo kutakuwa na maonyesho
mbalimbali ya bunifu za kisayansi na teknolojia.
Ameongeza kuwa kupitia Jukwaa hilo la Wiki ya ubunifu limekuwa
na mijadala mbalimbali inayochagiza maendeleo katika sekta ya ubunifu hususani
kwa vijana na kusavutia wengi zaidi, pia amesema wiki ya ubunifu imekuwa
ikiibua vipaji mbalimbali vya ubunifu.
Pia amesema Mwisho wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu kutakuwa na
tuzo za kuwatambua wabunifu mbalimbali waliofanya vizuri ambapo wiki ya ubunifu
itatamatika mei 24/2024.
Kupitia ubunifu vyombo vya habari vinaweza kusaidia zaidii katika kufikia malengo yanayotakiwa na vijana wengi wakafaidika zaidi na bunifu zao kwa kupata taarifa sahihi kuhusu ubunifu kupitia Vyombo vya habari.
Post a Comment