Ads

PURA NA ZPRA ZAKUTANA KUWEKA MIPANGO KUONGEZA UFANISI UTEKELEZA SEKTA YA GESI ASILIA

Watendaji wa  Bodi za Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli na Gesi Asilia (PURA) pamoja na Mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia Zanzibar (ZPRA) zimekutana na kuweka mipango na mikakati mbalimbali ya kuendeleza sekta ya Mafuta na Gesi asilia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya Mkutano wao Jijini Dar es salaam leo December 4/2023 Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni amesema amesema kuwa mkutano huo unashabaha ya kuendeleza sekta Mafuta na Gesi asilia.

"Leo hii tumekutana kujadili ,kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu ili tuweze kudhibiti na kuendeleza sekta hii muhimu kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa letu,tunatumaini baada ya kikao hiki tutaainisha mikakati yetu na kuifanyia kazi ipasavyo" amesisitiza Mhandisi Sangweni. 

Vilevile Mkurugenzi Mwendeshaji ZPRA Adam Makame amesema kwamba mkutano huo umenuia kuweka mazingira bora kwa pamoja nakuweza kutangaza vitalu vya Mafuta na Gesi asilia ili kuweza kupata wawekezaji wengi nakuwezesha kupata wawekezaji wengi katika sekta hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya PURA Alfan Alfan amesema kwamba ushirikiano wa PURA na ZPRA kutoka Zanzibar itasaidia kujenga mahusiano ya muda mrefu katika kuhakikisha wawekezaji wanapatikana Tanzania Bara na Visiwani.

"Ushirikiano huu utaleta manufaa makubwa kwenye bodi zetu hizi mbili(PURA na ZPRA ) tutaweza kutangaza vitalu vyetu nakupata wawekezaji wengi hivyo sekta ya Mafuta na Gesi asili itazidi kukua nakuleta maendeleo kwa Taifa letu"amesema Alfan.

Mwenyekiti wa bodi taasisi ya Utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar (ZPRA) Ali Mirza amesema kwamba kikao hicho kimefanyika kwa mara ya kwanza ili kujadiliana kwa pamoja nakuweka mikakati ya pamoja ya kunufaika na rasilimari ya Mafuta na Gesi asilia.

No comments