RC CHALAMILA ATOA SOMO KWA WAANDISHI WA HABARI ,TMDA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewataka wahariri wa vyombo vya habari na watendaji wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kutoogopa pindi wanapokutana na changamoto mbalimbali kwenye utendaji kazi wao hususani vitisho ili kulinda taaluma ya kazi zao.
Hayo ameyasema Leo Jijini Dar es Salaam wakati akifungua kikao kazi cha TMDA na wahariri wa Habari kuelezea mafanikio yake Kwa kipindi cha miaka 20 toka kuanzishwa kwake ambapo amesema ushirikiano wa pamoja katika utekelezaji wa majukumu utawezesha upatikanaji wa taarifa sahihi.
Aidha amesema mchango wa vyombo vya habari ni mkubwa katika kufikisha taarifa Kwa jamii hivyo ni vyema wahariri kabla ya kutoa taarifa za TMDA kuwasiliana nao nakujiridhisha Ili watoe taarifa yenye uhakika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Adam Fimbo amesema kwa kipindi cha miongo miwili katika usimamizi wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi, Mamlaka imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kufikia malengo yake kwa kuhakikisha jamii inalindwa afya zao na inakuwa salama kutokana na matumizi ya dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa nyinginezo zinazohusiana na afya.
Aidha ametaja mafanikio waliyopata ikiwemo mwaka 2011 Maabara ya TMDA kuwa na umahiri unaotambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO Prequlified Laboratory) 2012 kuwa Kituo cha umahiri wa usajili dawa barani Afrika na 2013 kuwa Maabara ya mafunzo ya umahiri kwa Mamlaka za Udhibiti Dawa barani Afrika.
Mafanikio mengine ni pamoja na mwaka 2014 Kuanzisha mifumo ya kielektroniki ya utoaji huduma Kwa wateja, 2015 Kutoa huduma za udhibiti kwa njia ya kielektroniki na Kuimarika kwa makusanyo hivyo kuchangia 15% ya mapato yake katika gawio la Serikali na kuwa na ziada ya 70% .
Hata hivyo mwaka 2017 wamefanikiwa Kuanzisha mazingira wezeshi na rafiki ya ufanyaji biashara nchini kwa bidhaa zinazodhibitiwa na TMDA, 2018 Kufikia Ngazi ya tatu ya Shirika la Afya Duniani - WHO kwa kuwa na mifumo bora ya udhibiti dawa barani Afrika hivyo kuwa taasisi ya kwanza ya udhibiti na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia ngazi hiyo na kupata hadhi ya juu ya ngazi ya nne umahiri wa Shirika la Afya Duniani (Quality Control LAB WHO ML 4).
Katika mafanikio hayo pia mwaka 2021 WiGo umeongezeka kwa Mamlaka kupewa jukumu la udhibiti wa bidhaa za tumbaku, 2022 Kuanzisha mfumo wa kufuatilia utoaji taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya dawa kwa njia ya simu pamoja na mamlaka kupata hati safi kwa miaka 20 mfululizo kufuatia ukaguzi wa hesabu za taasisi kwa ukaguzi unaofanywa na ofisi ya CAG.
Post a Comment