KATAMBI AAGIZA UZINGATIAJI USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI
Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amemtaka Meneja wa Kiwanda cha kutengeneza nguo 21st Centry ltd, bwana Tushpvir Singh kuzingatia usalama na afya mahali pa kazi kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Katambi amesema hayo Septemba 21, 2023 alipofanya ziara kiwandani hapo kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria za kazi, ajira na sheria ya afya na usalama mahali pa kazi.
Amesema wafanyakazi kutokuwa na vifaa kinga, mikataba isiyo rasmi, kufanya kazi kinyume na saa za kazi, maslahi hafifu ya wafanyakazi hali ambayo inahatarisha maisha yao.
Sambamba na hayo, amemtaka Meneja huyo kuzingatia kima cha chini cha mshahara kama kinavyoelekezwa katika sheria ya kazi.
“Kuna maeneo ambayo yanazalisha joto kali, kukaa katika maeneo ya joto muda mrefu kuna athari kubwa za kiafya unaweza kuzipata,” amesema.
Pia meneja wa kiwanda hicho bwana Puship Vir Singh amemshukuru sana Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu mhe.Patrobass Katambi kufika kiwandani hapo na kuahidi kwa yale ambayo amepewa maelekezo na serikali kuyatekeleza
Aidha meneja wa kiwanda hicho bwana Puship Vir Singh amemuomba mhe. Waziri serikali kuwatatulia baadhi ya changamoto wanazozipata kiwandani hapo kupelekea kukwamisha baadhi za kazi kiwandani hapo baadhi ya changamoto hizo ni umeme kukata mara kwa mara kupelekea kukwamisha kazi za kiwandani hapo,kutopata maji ya kutosha kiwandani hapo kupelekea kukwamisha kazi za kiwandani,changamoto nyingine ni kupanda kwa Kodi kupelekea vitu kupanda bei.
Uongozi wa kiwanda cha 21stCentury textile ltd unaishukuru sana serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa.
Post a Comment