KAMPUNI YA SILENT OCEAN YAFUNGUA OFISI NCHINI INDIA
Na Francisco Peter, Dar es Salaam
KAMPUNI ya usafirishaji wa mizigo ya Silent Ocean imefungua ofisi mpya Mumbai nchini India.
Hayo yamebainishwa leo Mei 16, 2023 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Mohammed Soloka wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi hiyo.
Soloka amesema wamefungua ofisi hiyo ili kusogeza huduma bora kwa wafanyabiashara wanaotoa bidhaa zao nchini India.
“India ni nchi ya pili duniani inayokua kwa kasi katika biashara na tuliona changamoto ya kuchelewesha kwa mizigo kufika nchini tukaamua kufungua ofisi hii,” amesema Soloka.
Amesema siku zote wapo na wafanyabiashara nakwamba hiyo ni fursa kwa Serikali kukusanya mapato na kukuza uchumi wa nchi kupitia ofisi hiyo na wafanyabishara watasafirisha mzigo kutoka India hadi Tanzania kwa siku 17 hadi 25 kwa muda mfupi.
Nae Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabishara Kariakoo, Abdalah Mwinyi amesema wanahaki ya kuwapongeza Silent Ocean kutokana na kurahisisha kufika kwa wakati mizigo ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
“Tuna kila sababu ya kuishukuru kampuni hii kwani kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita mizigo kufika nchini ilichuku muda wa miezi mitatu hadi sita, lakini kwa sasa mizigo inafika mapema," amesema Mwinyi na kuongeza
"Siku hizi mbili tunapitia kwenye wakati mgumu tunaimani kikao cha kesho na Waziri Mkuu kitaleta matunda, tunashukuru Silent Ocean kwa kuongeza tawi lingine,".
Naye Mwakilishi wa Wafanyabishara, Wahid Abdulghafoor amesema wafanyabishara wa nchi hizi mbili walikuwa na changamoto ya usafirishaji wa mizigo hivyo kwa sasa wanahitaji kufanya kazi na Silent Ocean.
Post a Comment