Ads

KAMISHNA WA ARDHI MKOA WA ARUSHA AWATAKA WADAIWA KULIPA KODI YA ARDHI.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Arusha Bw. Idrisa Kayera akizungumza katika kikao kazi na Wadaiwa wa kodi ya ardhi pamoja na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.

.............

Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Arusha Bw. Idrisa Kayera amewataka watu wote wanaodaiwa kodi ya ardhi kulipa kwa wakati, huku akibainisha kuwa Ofisi za ardhi  zitaendelea kuwahudumia wananchi kuanzia tarehe 29 hadi 30 Aprili mwaka huu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mhe. Waziri wa Ardhi Angeline Mabula kuwasilisha maombi ya kuongeza muda wa nyongeza  kwa Mhe. Rais  ili wadaiwa waweze kulipa kodi ya Ardhi bila ya riba, ambapo Mhe Rais aliridhia maombi hayo na kutoa ruhusa ya msamaha wa riba  hadi tarehe 30 April 2023.

Akizungumza katika kikao kazi na Wadaiwa wa kodi ya ardhi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Arusha Bw. Kayera, amesema kuwa msamaha huu ulitolewa hapo awali kwa kipindi cha miezi 6 toka Julai hadi Disemba 2022.

Kamishna Kayera amewakumbusha wajumbe wa kikao kuwa muda wa kulipa bila ya riba unaisha saa 6 usiku jumapili tarehe 30 April 2023.

"Sitegemei tena kusikia kutoka kwa wananchi kuwa hawajapata taarifa ya msamaha huo wa kodi na hivyo kuomba nyongeza ya muda" amesema Kamishna Kayera.

Kamishna Kayera amesema kuwa ofisi za ardhi katika Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha kuwa wazi kwa huduma kwa siku ya jumamosi na jumapili  tarehe 29 na 30 Aprili 2023

Hata hivyo Kamishna ametoa wito kwa Watendaji wa Halmashauri kwenda kwa wananchi kutoa elimu  wananchi kuhusu   kuacha kutumia maeneo ya barabara na kujenga kwa kuzingatia mpango miji.

"Wananchi mnapaswa kushirikiana na viongozi wa serkali za mitaa ili kupunguza migogoro ya mipaka ambayo imekuwa ikiripotiwa  Mkoani Arusha" amesema 

Kufatia uhamasishwaji huo kampuni tatu zilikuwa zinadaiwa Kodi zimelipa Sh 100,000,000.

No comments