Ads

Kila goli sasa milioni 10 Yanga Simba Kimataifa ,Poch la Mama linasuburia wafungaji tu.

 


Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza fedha za motisha kwa timu za Simba na Yanga kutoka shilingi milioni 5 hadi shilingi milioni 10 endapo timu hizo zitafuzu kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika na Kombe la Shirikisho barani Afrika.


Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Rais Samia anazitakia kila la kheri Simba na Yanga na amewataka wachezaji kujituma uwanjani na kutumia maarifa yao yote kuhakikisha wanashinda michezo ya kukamilisha robo fainali ili wafanikiwe kuingia nusu fainali ambapo kila goli litakuwa shilingi milioni 10.

Aidha, Msigwa amesema magoli yatakayolipiwa shilingi milioni 10 ni yale yatakayofungwa katika dakika 90 za mchezo au dakika 120 na sio magoli ya penati.

No comments