WAZAZI CCM ILALA ILIVYOJIPANGA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANAFUNZI NA WALIMU
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala, Mhe. Mtiti Jirabi akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Olympio, wakati akiwa katika ziara leo tarehe 9/3/2023.
Kamati hiyo ya utekelezaji inasimamiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mhe. Mohamed Msofe na Katibu wa Wazazi CCM Wilaya ya Ilala Mhe. Mtiti Jirabi akiwa mtendaji mkuu, ambapo lengo ni kutembelea shule zote za msingi na sekondari zilizopo Wilaya ya Ilala kwa ajili ya kuangalia utekelezaji
majukumu ya uongozi wa shule pamoja na kuhakikisha
watoto waansoma katika mazingira rafiki.
Akizungumza na
wanafunzi wa Shule ya Msingi Olympio Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala, Mhe. Mtiti Jirabi amewataka wanafunzi kuwa
na nidhamu jambo ambalo litawasaidia kuishi vizuri katika maisha yao na kupiga
hatua katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
“Tuepuke na vitendo
ambayo sio rafiki katika jamii, kwani Taifa linawategemea, waziri atatokea
hapa, Rais atatokea hapa, viongozi watatokea hapa someni kwa bidii” amesema
Mhe. Jirabi.
Katibu huyo ametumia fursa hiyo kueleza majukumu ya Jumuiya ya Wazazi Chama Cha CCM .
Mwenyekiti wa
kamati ya Shule ya Msingi Olympio Bw. Rajabu Amry, amesema kuwa kutokana na
mazingira ya shule watoto wanatoka mbali kuja kusoma katika shule hiyo.
Bw. Amry amesema
kuwa changamoto iliyopo watoto wanaishi mbali na shule na kusababisha kuchelewa
kufika shule kwa ajili ya kuendelea na masomo.
“Hatuna gari la shule kwa ajili ya usafiri wa wanafunzi, usafiri wanaotumia kwa sasa sio rasmi” amesema Bw. Amry.
Amesema katika
jitihada za kukabiliana na changamoto hiyo wamefanikiwa kuanzisha mradi wa ujenzi
wa gorofa nne katika shule hiyo.
“Katika gorofa nne
kutakuwa madarasa 11, ofisi tano, chumba cha huduma ya kwanza, chumba cha kuifadhia
vitu, kumbi za mikutano, Maktaba moja pamoja na
matundu ya vyoo 64.
Kamati ya
Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala
inatarajia kuendelea na ziara tarehe 10/3/2023 katika shule ya Sekondari
Jamhuri.
Post a Comment