Ads

GLOBAL PEACE WOMEN NA GLOBAL PEACE FOUNDATION TANZANIA ZAUNGANA NA TAASISI NYENGINE KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, YAGAWA TUZO KUTAMBUA MCHANGO MWANAMKE MWENYE ULEMAVU


Mkurugenzi wa Mfuko wa Udhamini wa Wanawake Tanzania (WFT- Trust) Rose Marandu (kulia), akimkabidhi Tuzo Mwanamke mwenye ulemavu katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliofanyika Katika Hotel ya Regency, Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Peace Foundation Tanzania  (GPF Tz) Martha Nghambi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Peace Foundation Tanzania  (GPF Tz) Martha Nghambi (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Udhamini wa Wanawake Tanzania (WFT- Trust) Rose Marandu katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliofanyika katika Hotel ya Regency, Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mfuko wa Udhamini wa Wanawake Tanzania (WFT- Trust) Rose Marandu akizungumza katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliofanyika katika Hotel ya Regency, Dar es Salaam.


Baadhi ya washiriki wakiwa katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliofanyika katika Hotel ya Regency, Dar es Salaam.

NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kufanya tafiti na  kuweka  mifumo thabiti ya uongozi ili wanawake wenye ulemavu waweze kuwa sehemu katika  kufanikisha mipango jambo ambalo litasaidia  kuona wapo wapi, wanamahitaji gani pamoja na kuyatambua mafanikio yao.

Akizungumza katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa mikutano Hoteli ya Regency, Mikocheni, Dar es Salaaam, Mkurugenzi wa Mfuko wa Udhamini wa Wanawake Tanzania (WFT- Trust) Rose Marandu, amesema kuwa ili kufikia mafanikio ya ajenda za wanawake zinapaswa kupewa kipaombele.

Mkurugenzi huyo Marandu ambaye ni mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo ameeleza kuwa "tunapaswa kujenga mifumo ya kuanzia ngazi ya familia ili tuweze kufikia nguvu za  kiuchumi, kuwa na meza za maamuzi, kuzijua haki na kupambana, kuiondoa mifumo kandamizi" 

Amesema kuwa katika juhudi hizo wanawake wenye ulemavu wapaswa kuwa sehemu ya utekelezaji   ili wasibaki nyuma na mabadiliko ya teknolojia na uchumi wa viwanda.

Hata hivyo kupitia mwanamke Hodari Awards 2023, wanawake wenye ulemavu wamepewa Tuzo katika Maadhimisho hayo kama sehemu ya kutambua mchango wao.

Tuzo hizo zimegusa nyanja za  michezo, kidigitali, ubunifu, wanaofanya uchechemuzi wa kuhakikisha haki za wanawake wenye ulemavu zinapatikana.

Hata hivyo  jamii inakumbusha kwa pamoja katika  kujumuisha wanawake wenye ulemavu katika kupanga pamoja na kufanya maamuzi ya shughuli mbalimbali kwani wao wamethibitisha  uwezo  na ndoto za kufika viwango vya juu ya  kuyafikia maendeleo.

Katika kufanikisha Maadhimisho hayo Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Global Peace Foundation Tanzania (GPF Tz) kwa kushirikiana na Mashirika wenza Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi Tanzania (FUWAVITA), Global Peace Women Tanzania, Darasa Tech, Mo dewji Fiundation na TSO wameungana kufanikisha tukio hilo muhimu.

Katika maadhimisho hayo  kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani  ikiwa   “UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA: CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA”

No comments