Ads

MLEZI CCM TAWI LA MTAMBANI A NA B ALIVYOMSAIDA MLEMAVU WA MIGUU.

Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi Mtambani A na Mtambani B katika Kata ya Jangwani Bw. Imran N. Jaffer (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mlemavu wa miguu  Bw. Nassor Amour baada ya kumkabidhi Kiti Mwendo  (wheelchair).

Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi Mtambani A na Mtambani B katika Kata ya Jangwani Bw. Imran N. Jaffer (kulia) akipongezwa na kiongozi wa CCM Kata ya Jangwani baada ya kutoa msaada wa kiti Mwendo  (wheelchair) Kwa mlemavu wa miguu.

Baadhi ya wanachama Cha CCM wakiwa katika tukio la Mlezi wa Tawi Mtambani A na Mtambani Bw. Imran N. Jaffer wakati akitoa msaada wa kiti Mwendo (wheelchair) kwa mlemavu  Bw. Nassor Amour.

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.

Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi Mtambani A na Mtambani B katika Kata ya Jangwani Bw. Imran N. Jaffer ameitaka jamii kuwa na utamaduni wa kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu hususani walemavu jambo ambalo litasaidia kupata baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuendelea kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo. 

Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati akitoa msaada wa kiti mwendo (wheelchair) kwa mlemavu wa miguu  Bw. Nassor Amour,  Bw. Jaffer  amesema ameguswa kumsaidia kijana huyo kutokana kwa muda mrefu ameshindwa kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyengine.

Bw. Jaffer amesema kuwa kutokana na hali yake kutokuwa vizuri ameona ni vizuri kumsaidia kama vitabu vitakatifu vinavyofundisha  tuwe na upendo na kuwasaidia watu wenye uhitaji.

"Niliwai kuwa mlemavu nilipokuwa mdogo, namshukuru Mungu baada ya kupata matibabu nilifanikiwa kupona na kurudi katika hali yangu ya kawaida" amesema Bw. Jaffer.

Hata hivyo amefafanua kuwa anatarajia kuendelea kutoa msaada wa viti mwendo  (wheelchair) kwa watu wenye ulemavu katika Kata ya Jangwani.

"Nimekuwa muumini wa kuwasaidia watu wenye uhitaji katika jamii lengo ni kuhakikisha  wanaishi katika mazingira rafiki" amesema Bw. Jaffer.

Bw. Jaffer amewataka wakazi wa Kata ya Jangwani kuwa na umoja kwani ni nguvu na unaleta mafanikio katika kufanikisha mipango mbalimbali ya kimaendeleo.

Bw. Imran N. Jaffer ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekuwa ni mtu rafiki kwa jamii kwani amekuwa akiisaidia jamii katika kutatua changamoto mbalimbali.

No comments