TANZANIA KUWA MWENYEJI MAONESHO SEKTA YA DAWA NA HUDUMA ZA AFYA.
TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa maonesho ya sekta ya dawa na huduma za afya kwa wadau na wataalam wa afya kutoka sehemu mbalimbali duniani yanatarajiwa kufanyika Desemba 14 hadi 16 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, Muandaaji wa Maonyesho hayo Thomas James amesema kuwa maonyesho hayo yatutoa nafasi kwa watanzania kubadilishana ujuzi wa dawa tiba na wataalamu wakubwa duniani.
"Maonyesho yatawakutanisha wazalishaji, wauzaji wa jumla, wafanyabiashara na wasambazaji wa sekta ya uchunguzi wa dawa, hospitali na watoa ushauri wenye ushawishi mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki nchini Tanzania.
Pia ameongeza kuwa Teknolojia imebadilika katika uchunguzi hasa utengenezaji wa dawa tiba imepelekea chama cha Phamasia kuandaa maonyesho ya dawa.
Katibu mtendaji wa MeLSAT Peter William amesema makampuni zaidi ya mia moja watashiriki maomyesho
Katika kuamasisha uwekezaji nchini kuna huhitaji wa kuwekeza kwenye viwanda vya hasa madawa.
Kwa upande wake Afisa Mwanachama kutoka TWCC Cresensia Mbunda, amesema kuwa maonyesho yatasaidia kunufaika na kuongeza uwekezaji kutokana na ujuzi tulioupata kupitia watu wa nchi mbalimbali.
“Maonyesho haya ni muhimu kwa nchi yetu kwani inakutanisha washiriki zaidi ya 90 kutoka mataifa mbalimbali ambao wataonyesha bidhaa zao, pia itaongeza ugunduzi na ubunifu wa bidhaa mpya na matukio katika sekta ya afya." amesema Cresensia
Maonyesho haya yameidhinishwa na Tantrade ikiwa na dhumuni la kutaka Watanzania wapate fursa ya kujifunza, kushirikiana na kuimarisha ushirikiano baina ya nchi zitakazoshiriki.
Post a Comment