MAKUBWA YA SIMBA TRAILERTS KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI , MKUTANO WA TAMSTOA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema imepokea changamoto ya kodi kwenye sekta ya usafirishaji (Provisional Tax) na kwenda kuzifanyia kazi jambo ambalo litasaidia kupunguza malalamiko na kuchochea chachu ya ukuaji wa sekta hiyo muhimu katika kukuza uchumi na kuongeza ajira kwa watanzania.
Akizungumza katika Mkutano wa Chama Cha Wamiliki wa Malori Madogo na ya kati (TAMSTOA), jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, amesema kuwa serikali kupitia wizara itaingalia kodi na kuja na mapendekezo sahihi ili kuendelea kuwa pamoja na wadau wa sekta ya usafirishaji na kuchochea maendeleo ya nchini.
Meneja msaidizi wa Kandarasi, Chama Cha Wamiliki wa Malori Madogo na ya kati (TAMSTOA), Abbas Dharamsi, amesema kuwa serikali kwa kupunguza malalamiko imesaidia kuongeza chachu ya uwekezaji kwenye sekta mbalimbali.
“Mkutano huu umekuwa na manufaa kwa sababu serikali kushirikiana na TAMSTOA na wadau wengine kwenye sekta ya usafirishaji wameweza kutafuta mapendekezo yatakayoweza kupunguza malalamiko ya wadau,”amesema Dharamsi.
Amesema kuwa Kampuni ya Simba imeweza kutoa matrekta imara kwa bei nzuri, kwani Simba Trailers ukaguliwa na na mafundi waliofunzwa ili kuhakikisha kila weld na sehemu zake zinakuwa katika hali nzuri kwa miaka mingi.
“Jisikie na uhakika kwamba Simba ina trela sahihi kwa kazi yako, trela hizi zinaweza kutosheleza mahitaji yao yote, iwe sebule, kontena, urefu wa 20.”
Amesema kuwa kampuni yao nyingine ya Simba Supply Chain Solutions wanauzoefu mkubwa wa miaka mingi katika usafirishaji barani Afrika.
Katika mkutano huo, serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imekubali ombi la Chama Cha Wamiliki wa Malori Madogo na ya kati (TAMSTOA) juu ya kodi kubwa katika kichwa na Trela na kodi hizo kuwa mzigo kwa wasafirishaji hapa nchini.
“Nachukua nafasi hii kuwaomba madereva wa malori hapa nchini kuendelea kuchapa kazi na endapo kuna matatizo yoyote basi wachukue njia za kisheria na za kiutaratibu kwa kuihusisha serikali na chama cha wamiliki wa malori ili kuhakikisha matatizo yao yanafanyiwa kazi kwa njia ya mazungumzo” amesema Dharamsi.
Hata hivyo imebainika kuwa changamoto ya maeneo ya maegesho ya malori kutoka Dar es Salaam hadi Tunduma serikali ipo katika hatua za mwisho kuanza mchakato na kupata uzabuni wa kujenga eneo la maegesho ya malori ili kuondoa atha wanaokuwa wanapata wamiliki.
Mwenyekiti wa TAMSTOA , Chuki Shabani, amesema kuwa wamiliki wa malori nchini wanapitia changamoto nyingi kwenye sekta hiyo ya usafirishaji ikiwemo faini za Mamlaka ya Usafiri wa nchini kavu (LATRA) na kuomba serikali kupitia wizara kuangalia namna nzuri ya kuendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwa maslahi mapana ya nchini.
“Ni matarajio yetu ombi letu kupitia kwa wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa kuangali upya kodi litafanyiwa kazi ili wamiliki wa malori waendelee kutoa huduma hii hapa nchini na nchini za jirani na kuchochea uchumi wa nchini na kuongeza kipato cha serikali,” amesema Shabani.
Amesisitiza kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana kama vile kuondoa migomo ya madereva na kuboresha huduma za mpakani Tunduma ila bado tatizo la usalama wa madereva katika nchini jirani hasa Zambia na Congo kwa sababu matukio ya utekaji wa madereva na malori bado yanaendelea na kuiomba serikali kuendelea kushirikiana na majirani zetu ili kuweza kutatua changamoto hiyo.
Post a Comment