Ads

WAMACHANGA WAIPONGEZA BENKI YA NMB KWA KUONESHA USHIRIKIANO KUWASAIDIA KIUCHUMI

 

Na Francisco Peter, Dar es Salaam.
Umoja wa Machinga nchini Tanzania (SHIUMA) imeipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kuonesha ushirikiano kwa  kuwasaidia kiuchumi katika kuhakikisha wanapiga hatua katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu juhudi za serikali katika kuwasaidia wamachinga,  Katibu wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam, Masoud Chauka, amesema kuwa uongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) umekuwa imara kutoa mrejesho kwa viongozi jambo ambalo limesaidia kuleta mafanikio.

“Tunajiandaa kufaidi  mikopo kutoka kwa benki ya NMB , kama katibu wa Mkoa huu, hivi karibuni nimeshiriki kikao na baadhi ya benki hapa nchini na wameonesha nia ya kutusaidia" amesema Chauka.

Amesema kuwa serikali imekuwa na mipango rafiki ya kuendelea kututengenezea  mazingira rafiki kwa  kujikwamua kwa kupata mikopo.

Amesema kuwa benki ya NMB inathamini juhudi za wajasiriamali wadogo kwa kuonyesha ushirikianoa katika kuhakikisha shughuli zao zinapiga hatua kimaendeleo.

"Benki ya NMB imewasaidia kwa kiasi kikubwa wamachinga katika masuala mbalimbali ikiwemo mitaji na fursa za kukuza biashara kwa miaka mingi" amesema Chauka.

No comments