SOMA HAPA KUJUA KUHUSU UJENZI WA BANDARI YA UVUVI KILWA.
MAANDALIZI ya awali ya ujenzi wa bandari ya uvuvi Kilwa Kivinje, mkoani Lindi yameanza, Bunge limeelezwa leo Dodoma.
Naibu Waziri wa Uvuvi, Abdallah Ulega ametoa maelezo na kuongeza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 24.
Kabla ya majibu hayo, Mbunge wa Kilwa Kusini, Ally Kassinge, ambaye kupitia swali lake la msingi, alitaka kujua lini mchakato wa kujenga bandari hiyo utaanza.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri, Mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo ulisainiwa Juni 7, 2022 kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi na mkandarasi ambaye ni Kampuni ya M/S China Harbour Engineering.
Akitoa ufafanuzi zaidi, Ulega amesema: “Serikali imeshaanza ujenzi wa Bandari ya Uvuvi katika eneo la Kilwa Masoko mkoani Lindi.
“Aidha, maandalizi ya awali ya ujenzi wa bandari hiyo yameanza na ujenzi unatarajia kukamilika ndani ya miezi 24.”
Post a Comment