RC MAKALA AKAGUA MTO RUVU HAYA NDIYO ALIYO YAKUTA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla leo ametumia usafiri wa chopa kukagua mito iliyopo Mikoa ya Pwani na Morogoro ambayo ndio chanzo cha maji Ruvu juu na chini.
Mkuu huyo wa mkoa amebaini uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu.
Makalla ameshuhudia kina cha maji kwenye Mito hiyo kikiwa kimeshuka jambo linalopelekea Mkoa wa Dar es salaam kukabiliwa na mgao wa maji.
Post a Comment