Ads

WABUNGE WAHOJI HAKI YA WAFUNGWA KUPATA FARAGHA YA TENDO LA NDOA

 

Na Mwandishi wetu - Bungeni


Serikali ya Tanzania imesema haki ya faragha kwa wafungwa na wenza wao itaanza kutolewa pale ambapo sheria na miundombinu ya magereza itakapokidhi kutolewa kwa haki hiyo

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni alipokuwa akijibu maswali ya baadhi ya wabunge waliohoji ni lini wafungwa watapata haki hiyo

Waziri Masauni amesema masuala mengine yatakayozingatiwa kabla ya kuruhusiwa ni usalama, mila na desturi za Tanzania kwani haki hiyo inatakiwa kutekelezwa kwa faragha

Aidha amesema serikali inaendelea kutoa haki nyingine za msingi kwa wafungwa ikiwemo malazi, mavazi na chakula

"Tendo la ndoa ni haki lakini sio haki ya msingi, haki ya msingi ambayo tunatoa kwa wafungwa ni chakula, mavazi, malazi. Kuna mambo mengi ambayo yanapaswa kufanyika kwanza kabla ya kuruhusu haki hiyo gerezani" amesisitiza Waziri Masauni


No comments