Ads

MALALAMIKO TISA YAJADILIWA NA BALAZA LA MAADILI

 

Kamishina wa Tume ya Maadili, Jaji wa Rufani Sivangilwa Mwangesi ,picha na maktaba ya mtandao.


Na.Wellu Mtaki.
Mwamba wa Habari


Balaza la maadili lipo Kwenye uchunguzi wa Malalamiko tisa toka sehemu mbalimbali, uchunguzi huo umeaza Tarehe 6 Septemba hadi tarehe16 septemba.
Hayo yamesemwa na jaji kamishina wa maadili 
Sivangilwa  Mwangesi wakati akizungumza na wahandiishi wa habari  jijini Dodoma.
Mwangesi amesema kamishina wa maadili ndiye anayepokea malalamiko toka sehemu tofauti tofauti na kuaza uchunguzi wa malalamiko hayo na baadaye kuyawasilisha malalamiko hayo kwenye balaza la maadili.
" Mpaka sasa kuna malalamiko tisa ambayo yanachunguzwa na balaza la maadili baada ya uchunguzi huo balaza litaandaa maoni yake kutokana na lalamiko lililotolewa na ushaidii ambao umepokelewa , uchunguzi huu unafanyika KWa mujibu wa kifungu cha 25(5)na 29(6) cha sheria ya maadili ya uongozi wa umma  ( sura 398)" amesema Mwangesi

Pia amesema balaza halitakuwa na siku ya kutoa ukumi  bali  litachua uamuzi wake kulingana na sheria ilivyo, litatoa ushauri baada ya hapo anakabidhiwa kamishina wa maadili  kwa ajiri ya kupeleka KWa mh rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Sekretariet ya maadili ya uongozi wa umma ni taasisi inayojitegemea chini  ya ofisi ya raisi iliyoanzishwa kwa mujibu wa idara ya 132 ya katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 1977 kutekeleza sheria ya maadili ya uongozi wa umma no. 13 ya mwaka 1995.
Jukumu kubwa ya taasisi hii ni kuchunguza tabia ya mwenendo wa kiongozi wa umma yoyote KWa madhumuni ya kuhakikisha mashart ya sheria ya maadili ya uongozi ya umma yanazingatiwa .

No comments