Ads

SERIKALI YATANGAZA UWEPO WA UGOJWA WA SURUA NCHINI

 



Wizara ya Afya nchini imetangaza kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa surua katika halmashauri saba huku watu 38 wakithibitika kuwa na ugonjwa huo.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Alhamisi Septemba 15,2022 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amezitaja halmashauri hizo kuwa ni Bukoba, Wilaya ya Handeni, Kilindi, Mkuranga, Kigamboni, Manispaa ya Temeke na Manispaa ya Ilala.

Aidha, amesema katika kudhibiti ugonjwa huo, wizara inaendelea kuimarisha ufuatiliaji wa wahisiwa kwa kutuma timu ya wataalamu kwenye maeneo yenye wagonjwa wengi na utoaji wa elimu kwa jamii.

No comments