Ads

RC SENYAMULE, AWAPONGEZA WANAWAKE WA KANISA LA AGLIKANA DODOMA ,KISA HIKI HAPA.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akizungumza wakati akiwaaga wake wa maaskofu wa makanisa ya Anglikana katika Kanisa la Anglikana Diocese ya Central Tanganyika ( DCT ) Agosti 25,2022 jijini Dodoma.

Askofu wa Diocese ya Central Tanganyika (DCT), Dickson Chilongani,akizungumza mara baada Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,kuwaaga  Wake wa maaskofu wa Makanisa ya Anglikana katika Kanisa la Anglikana Diocese ya Central Tanganyika (DCT) Agosti 25,2022 jijini Dodoma


Katibu wa umoja wa wanawake wake wa maaskofu Anglikana Askofu Agnes Liheli akizungumza na waandishi wa habari wa Dodoma mara baada ya mkuu wa Mkoa  Wa Dodoma Rosemary Senyamule kuwaaga wake wa maaskofu wa makanisa ya Anglikana katika kanisa la Anglikana Diocese ya Central Tanganyika ( DCT ) Agost 25, 2022 jijini Dodoma.

Na. Wellu Mtaki . DODOMA 

mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewapongeza wanawake wa kanisa la aglikana Wa Umoja  wa  Wake wa maaskofu wa Makanisa ya Anglikana (UWAKI)  kwa kujitoa kuunga juhudi za mh Rais Samia kwa kwenda ngorongoro kwa ajiri ya kufanya utalihi na amewasihi watumie safafi hiyo kama fursa kwao

Na ameliomba kanisa la Anglikana Mkoa wa Dodoma waendelee kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwa maarifa na utashi wa kuliongoza taaifa la Tanzania.


Ameyasema hayo wakati wa  kuwaaga Wake za Wachungaji pamoja na Maaskofu wa Kanisa la Anglikana Diocese ya Central Tanganyika (DCT) Agosti 25, 2022 Jijini Dodoma.


Amesema mapato ya Nchi yanategemea na utalihi, hivyo watumie fursa hii kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwani utalihi ni fedha, utalihi ni Burudani, Utalihi ni uchumi .



  KWa upandewake Askofu wa Diocese ya Central Tanganyika (DCT), Dickson Chilongani amesema safari hiyo ya Wake za Wachungaji na Maaskofu ni kwaajili ya Kuunga Mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kukuza na kutangaza utalii ndani na nje ya Nchi yetu pamoja na kwenda kujifunza fursa mbalimbali zilizopo kwenye mbuga hiyo


" Jumla ya Wake za Wachungaji na Maaskofu wanaokwenda Ngorongoro ni 100 imeandaliwa safari hii ni KWa ajiri ya kuunga jitiada ya mh. Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani"


" Hii ni awamu ya kwanza ambao wanakwenda  lakini kuna awamu kama tatu kwasababu tuna Wake za Wachungaji pamoja na Maaskofu 300 na jitihada za Rais zitaendelea kuzaa matunda kupitia Utalii wetu".Amesema Chilongani


Naye Agnes Riheli ambae ni Mchungaji na Katibu Idara ya Diocese ya Central (DCT)Tanganyika  amesema kuwa wazo hilo la kutembelea mbuga ya Ngorongoro kulilikuwa na muitikio mkubwa sana mara baada ya Taarifa kutolewa watu waliaza kutoa michango.


"Hili ni wazo ambalo kila mtu alilipitisha na moja kwa moja likapelekwa KWa  Baba askofu na muhitikio ulikuwa mkubwa, safari hii ni wanawake tumejiwezesha japo na kanisa wametuchangia


" Sisi Wanawake wa Dayosisi hii tupo wengi ni zaidi ya 300 na tumeweka utaratibu tutakapo rudi tutaratibu safari nyingine na kila Mtu atakwenda na Tunatamani katika ziara hii tuwe mfano kwa Watu wengine kwasabau tunamuunga Mkono Rais wetu Samia Suluhu". Amesema Riheli


 

No comments