Ads

PURA YAENDELEA KUTOA ELIMU KUHUSU GESI ASILIA (LNG) KATIKA MAONESHO YA BIASHARA SABASABA.

 


Mhandisi Charles Sangweni  ambambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa PURA, akizungumza na waandishi wa habari katika banda Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA),katika Viwanja vya Julius Nyerere Sabasaba  Kilwa road DSM.

Na. Mwamba wa habari sabasaba

Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni imesema iwapo hakutakuwa na vikwazo, uzalishaji wa Mradi wa Kuchataka Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) katika Mkoa wa Lindi utaanza mwaka 2025 na gesi ya kwanza itaanza kuuzwa 2030.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mkuu  wa mamlaka hiyo Mhandisi Sangweni  wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 46  Sabasaba yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere Kirwa road.

Amesema Juni 11 mwaka huu walifanya makubaliano ya awali ya mkataba husika, kama majadiliano ya muundo wa mradi, ukubwa wa mradi, sheria iweje na kwamba majadiliano yakikamilika wanatarajia Desemba 8 mwaka huu watasaini mkataba uliokamilika.

Mkurugenzi huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Majadiliano amesema baada ya mkataba rasmi kukamilika wanatarajia kwenda kwenye kazi ya usanifu wa mradi na namna ya kupata fedha za utekelezaji.

Mhandisi huyo alisema iwapo hakutakuwa na changamoto katika mradi huo unaogharimu zaidi ya Sh.trilioni 70 utaweza kuzalisha gesi asilia kwa  miaka 30.

Alisema katika kipindi cha ujenzi wa mradi huo zaidi ya ajira 10,000 zitapatikana na ajira za kudumu zitakuwa zaidi 600 pamoja na kuchochea shughuli nyingine za kiuchumi kwenye eneo la mradi.

Mkurugenzi huyo alisema tafiti zinaonesha kuwa utekelezaji wa miradi mikubwa kama hiyo ikifanyika katika nchi kama Tanzania pato la taifa litaongezeka kwa asilimia 1.5.

Msanweni amesema baada ya mradi huo kuanza kuzalisha gesi asilia wanatarajia kuuza katika nchi za Mashariki ya Mbali kama Japani, China na nyinginezo ambazo zimeonekana kuhitaji.

Aliwataka wawekezaji wa Kitanzania na wengine kujipanga vizuri katika kutumia fursa zitakazokuwepo katika mradi huo, akitolea mfano kuwa nondo, saruji na bidhaa nyingine zitahitajika.

Mwenyekiti huyo amesema watajitahidi kuandaa mazingira wezeshi ili Watanzania wawe kwenye viwango ambavyo vinakubalika katika miradi mikubwa kama hiyo.

Alisema wamekuwa wakkifanya mikutano na wadau mbalimbali kama wakuu wa taasisi waweze kujiandaa kushiriki katika mradi huo ambao unaenda kuleta mapinduzi ya kiuchumi, kijamii na maendeleo.

Mkurugenzi huyo alisema azo la mradi huo lilinza mwaka 2012 ila kuna changamoto zilizotokea, lakini kwa sasa Rais Samia Suluhu Hassan ameamua kuendeleza na matarajio yao ni mradi kutekelezwa kwa viwango vinavyokubalika.

PURA pia ndiye  mshauri wa Serikali kuhusu shughuli za mkondo wa juu,  kuthibiti na kusimamia Mradi wa LNG.

Amesema utekelezaji wa mradi huo ujenzi wake utaanza mwaka 2025 na unatarajiwa kukamilika  katika kipindi cha miaka mitano utakuwa umekamilika na gesi ya kwanza itaanza kutoka 2030.

Pamoja na hayo amewakaribisha watu wote kutembelea banda la PURA ili waweze kupata elimu zaidi kuhusiana na mamlaka hiyo.

No comments