Ads

MUHAS YADAHILI WANAFUNZI ZAIDI YA ELFU 9 TANGU KUFUNGULIWA KWA DIRISHA HILO

 

Na: Hughes Dugilo, DAR.

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimesema kuwa tangu kufunguliwa kwa Dirisha la Udahili wa wanafunzi wa Elimu ya Juu Chuo hicho kimefanikiwa kudahili wanafunzi zaidi ya elfu tisa.

hayo yamebainishwa na Afisa Uhusiano wa Chuo hicho Neema Edwin katika mahojiano maalum na waandishi wa habari wakati wa kufunga rasmi Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu sayansi na Teknolojia yalimalizika leo Julai 23,2022 katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Chuo hicho kimeshiriki kwa mafaniko makubwa maonesho hayo ambapo pamoja na mambo mengine kimepata fursa ya kutembelewa na watu wengi hususani wanafunzi wanaotaka kujiunga na Chuo hicho ambapo pamoja na mambo mengine walifanya udahili wa papo wa hapo katika maonesho hayo.

Adha  idadi hiyo ya wanafunzi zaidi ya elfu tisa imejumuisha na wale waliodahiliwa katika maonesho hayo na kwamba wanafunzi wanaoomba kujiunga na Chuo hicho wanaendelea kufanya maombi ya moja kwa moja kupitia mtandao wa Chuo hicho wa www.oac.muhas.ac.tz ambapo kwa kupitia tovuti hiyo mwanafunzi anaweza kujisajili mwenye akiwa mahali popote.

"Katika maonesho haya tumetembelewa na watu zaidi ya 500 ambao wamefika hapa kupata maelezo mbalimbali juu ya chuo chetu na wengi wao wamefanya udahili wa moja kwa moja  hapa"  Amesema Neema.

Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yalifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu Kassim majaliwa Majaliwa  Julai 18 ambapo leo Julai 23,2022 yamefungwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Dkt. Francis Maiko.

No comments