WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII ATOA AGIZO LA MIKOA YOTE KUIGA MFANO WA MKOA WA SHINYANGA KATIKA KUJENGA VIJIJI VYA MAONYESHO YA  UTAMADUNI KWA AJILI YA MAKABILA YAO

Agizo hilo limetolewa siku ya Leo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Pindi Chana wakati alipokuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye ufunguzi wa Kijiji Cha Utamaduni kilichofanyika katika Mkoa wa Shinyanga

Ambapo Mheshimiwa Waziri amesema anamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Sophia Mjema kwa ubunifu mkubwa alioufanya wa kutii na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kila Mkoa unaenzi na kudumisha tamaduni zao hivyo Mkuu wa mkoa akaamuwa kufanya ubunifu mkubwa wa kuhakikisha amejenga Kijiji ambacho kitakuwa ni maalumu katika kuenzi na kudumisha utamaduni wa makabila yote yaliyopo katika Mkoa huo yanadumishwa na kuenziwa vizuri

Aidha Mheshimiwa Pindi Chana ametoa wito kwa Mikoa yote nchini kuiga mfano uliofanywa na Mkoa wa Shinyanga katika kujenga vijiji na kuenzi makabila na tamaduni zao zote hivyo akatoa msisitizo wa jambo Hili kuhakikisha Mikoa yote imefanya na kuhakikisha inadumisha vyema tamaduni  na kabila zote zilizopo katika Mikoa

'Natoa agizo kwa Mikoa yote nchini kuhakikisha inaiga mfano huu ambao umeandaliwa na Mkoa wa Shinyanga ni ubunifu mzuri mno ambao tumejionea ni kwa namna gani Machief na watemi zamani walivyokuwa wakiishi na maisha yao halisi pia mpangilio mzuri wa Kijiji kimoja ambacho kimekuwa na maonyesho ya tamaduni kwa wilaya zote zilizopo katika Mkoa huu hivyo nahitaji Mikoa mingine yote ifanye ubunifu huu ili tuweze kuona makabila yao na tamaduni zao zikienziwa na hili ndilo agizo la Mheshimiwa Rais wetu' amesema Waziri

Sambamba na ufunguzi huo wa Kijiji Cha Utamaduni kwa Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Waziri alizindua pia filamu ya Royal Tour kwa Mkoa wa Shinyanga iliyochezwa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mama Samia Suluhu yenye lengo la kutangaza Vivutio vya Utalii vilivyopo nchini pamoja na kuitangaza Tanzania kimataifa zaidi

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Sophia Mjema amesema anajivunia na anaona ufahari mkubwa kwa jinsi na namna machief na watemi katika Mkoa huo walivyojitoa katika kuhakikisha wanafanikisha vyema zoezi Zima la kuonyesha utamaduni kwa Mkoa linafanikiwa vyema

Aidha ameongeza kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia kwa jinsi anavyoipeperusha vyema Bendera ya Tanzania katika kuhakikisha kila mwananchi anafurahia matunda ya Nchi yake sambamba na kuitangaza nchi kimataifa.