DC LUBIGIJA AKUTANA NA WATENDAJI SERIKALI ZA MTAA KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA YA ARIDHI.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Bwilaguzu Lubigija ameyataka Makapuni ya Urasmishaji wa Ardhi
kutekeleza Majukumu yao kwa weledi.
Akizungumza katika kikao Cha Wenyeviti wa Serikali za mitaa na Watendaji wa Ardhi jijini Dar es Salaam Bwilaguzu Lubigija amesema wale watakao bainika makampuni yao hayatafanya kazi kwa weledi watachukuliwa hatua.
"Kampuni zinazolalamikiwa nazitaka kuja kwenye kikao Jumanne ijayo watakaoshindwa nitatumia nguvu zaidi kuwapata". amesema Lubigija.
Lubigija amesema ili
wananchi waweze kutumia hati zao kuweza kupata mikopo katika taasisi za kibenki.
Aliongeza kampuni za
kihuni zilizochukua fedha na kushindwa
kufanya kazi zitachukuliwa hatua za kisheria.
"Katika zoezi hilo
la Urasmishaji linatupelekea katika
kupata hati". alisisitiza.
Ametoa wito kwa wananchi
kujitokeza kushiriki zoezi la urasmishaji wa ardhi katika maeneo yao.
Kaimu Kamishina wa
Ardhi wa Mkoa wa Dar es Salaam Idrisa kayela, ametoa wito kwa wananchi
kujitokeza kushiriki zoezi la urasmishaji wa ardhi katika maeneo yao na amesema
jumla ya viwanja 2,28000 vimetambuliwa kati viwanja 6000,00 na hati 4000
zimetambuliwa.
"Mikakati ni
kumilikisha mitaa hati 105 ambapo kumekuwa na ushirikishwaji mdogo".
Amesema kayela.
Kayela amesema kuwa
kumekuwa na changamoto ya baadhi ya watalamu ambapo kumekuwa na maeneo yamepimwa lakini
kumekuwa natatizo la uthibitisho wa umililiki wa ardhi.
Aliongeza kuwa kumekuwa
changamoto ya Elimu na uhudhuriaji wa Mafunzo ya Urasmishaji.
"Zoezi hili lilianza
Mwaka 2013 linatarajiwa kumalizika 2025 kwasasa Gharama imeshuka kutoka
shilingi 150000 Hadi kufikikia shilingi 130,000'". Alisisitiza Kayela.
Kayela alibainisha kiasi
kilichokusanywa nishilingi bilioni 22 huku lengo likiwa ni bilioni 79.
Post a Comment