Waziri wa fedha awasilisha muswaada wa sheria ya fedha.
DODOMA
Waziri wa Fedha na Mipango, Dakta Mwigulu Nchemba leo amewasilisha bungeni muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2022, jijini Dodoma .
Mwigulu amependekeza kuongeza wigo wa kusamehe tozo ya mafunzo ya ufundi stadi kwa wahitimu wa elimu ya juu na vyuo vya kati badala ya vyuo vikuu pekee kama alivyopendekeza hapo awali kwenye Hotuba ya Bajeti.
Amesema Lengo la hatua hii ni kuongeza idadi ya wanufaika wa mafunzo ya vitendo ya kuwapatia ujuzi na uzoefu wa kazi kabla ya ajira kupitia Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (Taesa).
Aidha Dakta Mwigulu Nchemba amependekeza bungeni kufanya marekebisho katika Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, Sura ya 197 kwenye vifungu vya 35(2) na 36(1) ili kuongeza kiwango cha ukomo wa Serikali kukopa kutoka Benki Kuu.
Lengo la marekebisho haya ni kuiwezesha Serikali kutekeleza Bajeti zake kwa ufanisi hususan kwenye kutekeleza miradi ya maendeleo.
Post a Comment