WAZIRI NAPE NAUYE ATOA PONGEZI KWA SHIRIKA LA POSTA NA TUTUME KWA KUONGEZA UBUNIFU.
Shirika la posta nchini pamoja na Kampuni ya kusafirisha mizigo ya TUTUME wamepongezwa kwa ubunifu wa kushirikiana kuhakikisha watanzania hawakosi huduma muhimu za afya.
Pongezi hizo zimatolewa na
Waziri wa Habari, Mawasialiano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Moses Nauye
alipoalikwa kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa usafirishaji wa sampuli za
kibaiolojia baina ya shirika hilo pamoja na kampuni hiyo.
Aidha amesema kuwa kama
lilivyo lengo la serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan la
kusogeza huduma mbalimbali karibu na wananchi hivyo mikataba hiyo itasaidia
sana kupanua huduma hizo hasa katika upende wa Afya.
Ameongeza kuwa licha ya kuwa
mkataba huo unalenga sekta lakini angalieni pia katika maeneo mengine ambayo
mnaweza kushirikiana na mkiangalia wote mnafanya kazi ya aina moja hivyo
mkiongeza mashirikiano katika vitu vingi mtaweza kuwasaidia watanzania kwa
sehemu kubwa sana.
Amemalizia kwa kuwataka
TUTUME, Shirika la Posta pamoja na wote wanaotoa huduma za kusafirisha bidhaa
kuweza kuutumia vizuri mfumo wa anuwani za makazi ili kurahisisha ufanyaji wao
wa kazi, na pia amewaomba Wizara ya Afya ikiwezekana kuwafuata watu majumbani
kuchukua sampuli na kutuma kwa mashirika haya na baadae kuwarudishia pia majibu
kupitia wasafirishaji hao hao.
Posta Masta Mkuu wa
Shirika la Posta Tanzania (TPC) Macrice Mbodo amesema kuwa mkataba huo
waliyosaini na Kampuni ya TUTUME ni wa kiuwakala wa kusambaza Sampuli
mbalimbali za Mahabara
Ameongeza kuwa majukumu ya
TUTUME, itakuwa ni kuchukua Sampuli kutoka katika ngazi ya kwanza ya Mahabara
na kupeleka ngazi ya pili ya Mahabara na wao Shirika la Posta kazi yao itakuwa
ni kutoa ngazi ya pili na kupeleka katika Mahabara za uchunguzi na baadae
muhusika kupelekewa majibu yake.
Ameendelea kusisitiza kuwa
Shirika la Posta limekuwa likitoa huduma za kusafirisha mizigo kwa njia mbili
yaani njia ya haraka pamoja na kawaida, Na kuongeza kuwa mpaka sasa shirika
hilo limetoa ajira ya uwakala kwa vijana wa boda boda zaidi ya 450.
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Tutume, Misana Manyama amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka
mazingira wezeshi kwa sekta binafsi zinapohitaji kushirikiana na idara za
Serikali ili kuweza kuleta maendeleo katika nchi yetu.
Post a Comment