WAZIRI MKUU MGENI RASMI UZINDUZI TAMASHA LA UTAMADUNI SIKU YA KISWAHILI DUNIANI
Na Francisco Peter
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Tamasha kubwa la Kwanza Kitaifa la Utamaduni na Siku ya Kiswahili Duniani litakalofanyika Kuanzia Julai Mosi Mwaka huu jijini Dar es salaam lenye ujumbe usema" Utamaduni Wetu;Fahari yetu;tujiandae kuhesabiwa ,Kazi iendelee.
Akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa huo Amos Makala amesema kwamba
Tamasha hilo litafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia Julai 1 hadi Julai 3
Mwaka huu ikiwa lengo ni kuifanya jamii kutambua,kuthamini na kuendeleza urithi
na Utamaduni waliorithi kutoka kwa wazazi na kuenzi lugha ya Kiswahili.
"Kuandaliwa Kwa
Tamasha hilo ni utekelezwaji wa maagizo ya Mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassani aliyoitoa Mkoani
Mwanza Septemba 8 Mwaka 2021 katika Tamasha la Utamaduni Mwanza ambapo aliagiza
matamasha yafanyike Kwa mzunguko kila Mkoa na washindi wapatiwe tuzo"
amesema RC Makalla.
Naomba ninukuu agizo la
Mh. Raisi " Matamasha haya yafanyike kwa mzunguko kila Mkoa ili Watanzania
waweze kujua mila na desturi zetu za kila Mkoa na kila pembe ya Tanzania ,pia
kuandaa mashindano yatakayoshindaniwa na Mikoa yote ambapo mshindi atapata
Tuzo,mwisho wa kunukuu" ameongeza.
Hali kadhalika amendelea kufafanua kuwa kutakuwa na matukio
mbalimbali yatakayohusishwa kwenye tamasha hilo
ambapo Julai 1-3 Usiku wa taarabu katika fukwe za coco(Coco Beach) ikihusisha
wasanii nguli akiwemo Khadija Kopa, Isha Mashauzi,Patricia Hilary pamoja na
vikundi kutoka Safina Modern Taraabu,First Class,Nakshi Nakshi pamoja Vikundi
kutoka nje ya Nchi za Burundi,Kenya,na Visiwa vya Comoro.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar
es salaam amesema kwamba baada ya Julai
4 kutakuwa na maandamano ya amani kutoka Wilayani Temeke hadi uwanja wa Uhuru jijini
hapa,nakwamba yatahusu lugha ya kiswahili
na utoaji wa haki na yataongozwa na Waziri wa katiba na Sheria Dkt Damasi Ndumbaro.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Lugha kutoka Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt Mnata Resani amesema kuwa
Julai 6 kutakuwa na kongamano linalohusu mchango wa kugha ya Kiswahili katika
harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika na mchokoza mada katika kongamano hilo ni Balozi Mstaafu Ame Mpungwe pamoja na viongozi
kutoka nje ya Nchi.
"Kama mnavyofahamu
UNESCO imeipa lugha ya kiswahili heshima kwa kuipa siku yake ya kuiadhimisha
ambayo ni Julai 7 kila Mwaka, hivyo Tanzania ambayo ndiyo yenye Johari hii
kiswahili imeandaa Maadhimisho ya siku ya kiswahili Duniani (MASIKIDU)
itaadhimishwa mara ya kwanza
Duniani"amesema Dkt Resani
Ameongeza kuwa Julai 7
mwaka huu Kwa mara ya kwanza ni maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani ,huku kitaifa tukio linatarajiwa kufanyika katika Viwanja
vya Uhuru jijini Dar es salaam
,nakwamba mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Rais Samia Suluhu Hassani.
"Kiswahili ni lugha
pendwa na imekuwa ikizidi kuenea Duniani kote hivyo baraza la kiswahili
limekuwa na utaratibu wa kuwatambua wataalamu wa lugha hiyo Kwa kuanzisha kanzi
data ili wajisajili lengo ni kujua takwimu
yao" amesisitiza Dkt Resani.
Hata hivyo ametumia fursa
hiyo kutoa with kwa Wananchi kushiriki
katika matukio hayo ya kihistoria ,ambapo pia wageni kutoka nje ya nchi ya Tanzania watakuwepo
kuja kuunga mkono siku ya kiswahili
duniani ,nakwamba marais wastaafu
Joachim Chisano kutoka Msumbiji pamoja na Sam Nujoma kutoka Namibia watahudhulia katika
maadhimisho hayo.
Post a Comment