TTCL KUPITIA T-PESA YAUNGANA NA KAMPUNI YA NGASMAKE KUZINDUA HUDUMA YA LIPA KWA UHAKIKA.
Akizungumza na wanahabari
leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa T-PESA, Lulu Mkudde amesema huduma hiyo
itaenda kuwa suluhisho la wanunuzi na wauzaji wa bidhaa kwa njia ya mtandao
kwani itasaidia kuondoa utapeli na udaganyifu kwa watumiaji.
"T-PESA kwa
kushirikiana na NGASMAKE kwa pamoja tumefanikisha kuwezesha huduma hii ya LIPA
KWA UHAKIKA ambayo ni pekee kabisa inayowahakikishia usalama wa bidhaa
zao," amesema Lulu.
Amebainisha kuwa huduma
hiyo iataondoa kilio cha muda mrefu cha wanunuzi wa bidhaa kutopata bidhaa zao
ingawa wamefanya malipo, kwani muuzaji atatsubiri mapka mnunuzi apate bidhaa
yake ndio fedha itaingia kwenye akaunti yake.
Amesisitiza kuwa mfumo
utamsiadia mnunuzi fedha zake kuwa salama
hadi atatakopata bidhaa au huduma na kwamba anaweza kurudisha malipo
yake ikiwa bidhaa haijawasilishwa.
Ameongeza kuwa Muuzaji
tafaidika kwa uwepo wa mfumo huo kwani atakuwa na uwezo wa kiuhakika wa malipo
mara tu wanapowasilisha bidhaa au huduma hivyo anauwezo wa kupokea taarifa ya
malipo kabla hajatoa huduma.
Ametoa rai kwa wanunuzi wa
huduam au bidhaa kupitia mitandao ya kibiashara inayopatikana nchini kutumia
mfumo huo sababu unatoa usala wa fedha za wateja huku akiwakumbusha huduma hiyo
inapatikana kwa kupiga menyu *150*71# kisha kuchagua namba 4 yenye Huduma ya
Lipa Kwa Uhakika.
Kwa upande wake,
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NGASMAKE, Emmanuel Ngalya amesema kampuni
hiyo inatoa huduma ya mfumo wa kifedha unaomlinda muuzaji na mnuunuzi kwa pamoja na kwamba
kutokana na changamoto nyingi za kiusalama katika biashara ya kimtandao ikiwemo
utapeli na udanganyifu wamekuja na mfumo rafiki na salama wa LIPA KWA UHAKIKA
utakaosaidia kuondoa changamoto hizo na kupata bidhaa zisizo na kiwango.
Amefafanua kuwa mfumo huo
unafanya kazi, mnunuzi baada ya kununua
bidhaa na kulipia T-PESA fedha
hazitaenda moja kwa moja muuzaji zitahifadhiwa
kwenye mfumo mpka pale mnunuzi atakapopata bidhaa yake na kuthibitisha
bidhaa aliyoagiza ndio mfumo utaruhusu fedha hizo kwenda kwa muuzaji.
Mkurugenzi mtendaji huyo
amesema mfumo huo umewekwa vizuri kwa watumiaji na endapo watapata changamoto
yoyote ya aidha kukosa huduma watapiga namba maalum ya kituo cha huduma kwa
wateja 0800110137 au kurasa za mitandao ya kijamii.
Post a Comment