Ads

Spika Dakta. Tulia amemuonya Mbunge wa Tarime Vijijini

 


Spika Dakta. Tulia amemuonya Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara kwa utovu wa nidhamu kwa kushindwa kufuata kanuni za Bunge na badala yake kwenda kulalamika gazetini kuhusu madai ya Wananchi Jimboni kwake kudaiwa kuuawa na Watu wa hifadhi ya Serengeti.

Dakta. Tulia ametoa onyo hilo hilo bungeni Dodoma leo June 14 2022 baada ya kipindi cha maswali na majibu na kusema Waitara akutaka kufuata kanuni kama hakuridhika na uamuzi wa Spika kwa kuwasilisha malalamiko yake kwa katibu wa bunge ili yafanyiwe kazi badala yake alienda kulalamika kwenye vyombo vya habari juu ya uamuzi wa Spika.

June 4 2022 Spika alitoa maagizo kwa wabunge Mwita Witara na Philip Mlugo kupelekea ushahidi wa malalamiko waliyoyatoa ndani ya bunge, hata hivyo baada ya kuwasilisha kwa Spika alisema mawasilisho hayakuwa tofauti na madai na hayakuweza kuthibitisha tuhuma zao hivyo Spika aliielekeza Serikali kufanya uchunguzi na kuleta majibu ndani ya siku 90.

Leo Spika Tulia amemnukuu Mwita Waitara kama aliyonukuliwa kwenye gazeti la Raia Mwema akisema " ni vigumu Serikali inayotuhumiwa kutenda jambo fulani kwenda kujichunguza na badala yake bunge lilipaswa kuunda kamati teule kuchunguza na taarifa inapaswa kuwasilishwa kwake si kama alivyoifanya Spika"

No comments