RC MJEMA AZINDUA KAMPENI YA TRA ELIMU YA KODI MLANGO KWA MLANGO KWA WAFANYABIASHARA WOTE MKOA WA SHINYANGA.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Sophia Mjema siku ya Leo amezindua kampeni iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kutoa elimu ya kulipa Kodi kwa wafanyabiashara wote waliopo katika Mkoa wa Shinyanga
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kampeni hiyo Mheshimiwa Mjema ametoa wito kwa wafanyabiashara wote waliopo katika Mkoa mzima wa Shinyanga kuhakikisha wanajitokeza na wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa Maafisa hao wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kila wanapokuwa wamepita katika sehemu zao za biashara na katika ofisi zao.
Hata hivyo ameongeza kuwa Kampeni hiyo itasaidia katika kuhakikisha Mkoa mzima wa Shinyanga unakuwa mstari wa mbele katika kulipa Kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa
‘Natoa wito kwa Wananchi wote ambao wapo katika Mkoa huu wa Shinyanga kila wilaya, kata,vijiji hususani kwa sehemu zote ambazo biashara zinafanyika, kila mfanyabiashara atoe ushirikiano wa kutosha kwa Maafisa Hawa wa (TRA) lengo tunahitaji Mkoa wetu kila mfanyabiashara apate elimu ya mlipa Kodi kusudi apate kufahamu umuhimu wa kulipa Kodi kwa Taifa lake’ amesema RC Mjema
Sanjari na Hayo Mheshimiwa Mjema ametoa wito kwa Wananchi wote Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi siku ya Sensa ya watu na Makazi tarehe 23.08.2022 kwa ajili ya kuhesabiwa ili kuweza kuwekewa mazingira mazuri ya kimaendeleo
Kwa upande wake Afisa Mkuu msimamizi wa Kodi Mamlaka ya Mapato (TRA) Bwana Edwin Lwato amesema Kutoa elimu kwa wafanyabiashara hususani wa mkoa wa Shinyanga kutasaidia katika kuongeza na kutimiza lengo la Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kukusanya Kodi pamoja na kutimiza lengo la Serikali katika kuwahudumia Wananchi kwani bila kulipa Kodi Serikali haiwezi kupata fedha za Maendeleo
Kampeni hiyo itaendeshwa kwa muda upatao mwezi mmoja Toka kuzinduliwa kwake siku ya Leo tarehe 03.06.2022 na zoezi hilo litaendeshwa kwa Mkoa mzima wa Shinyanga.
Post a Comment