Ads

URUSI YAISHUTUMU MAREKANI KWA KUTAKA KUIFANYA DUNIA KIJIJI CHA CHAKE

 


Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov amewakosoa Marekani kwa Propaganda zao kwa kukosoa mpango kazi wao wa dunia uitwao "US VISION FOR THE WORLD".


Mpango huu wa Marekani unahusisha na kuifanya dunia iwe kama kijiji "GLOBAL VILLAGE". Sasa waziri huyu amewakosoa kwa kusema lengo lao si kuifanyia dunia iwe kama kijiji badala yake ni kuifanya dunia iwe kama kijiji cha Marekani "AMERICAN VILLAGE" au "AMERICAN SALOON" yaani wanataka kuimiliki dunia.

Alisisitiza kwamba wao kama Russia hawatakubali kuongozwa na Marekani ndo maana wanapambana kuondoa vibaraka wa Marekani katika ukanda wao pamoja marafiki wenzake wa umoja wa ulaya na jeshi zima la NATO.

Waziri huyu pia aliongeza kwa kuonesha masikitiko yake ya wazi na kuzikosoa Media za Magharibi na Marekani kwa namna wanavoandika habari za kutunga na propaganda za kuichafua Russia kama nchi inayofanya ugaidi.

Alimaliza kwa kusema kwamba mara zote wamekuwa wakijitegemea wao wenyewe katika masuala mengi muhimu ya kiafya, elimu, maendeleo na uchumi pia hivyo watashirikiana na nchi rafiki wa Russia ili kuendelea kujijenga kiuchumi kama ilivyo kawaida na utamaduni wao.











No comments