TBS YAWAJENGEA UWEZO WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI.
Shirika la Viwango Tanzania –TBS limewataka
waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuwasisitiza wataalamu mbalimbali kuwa
uandaaji wa viwango ni wa shirikishi lengo ni kutoa uhakikisho wa ubora, usalama,
kuaminika na ufanisi.
Hayo yamesema leo tarehe 21/3/ 2022 jijini Dar es salaam katika mkutano
baina ya Shirika hilo na wahariri wa vyombo vya habari ambapo imeelezwa kuwa
wanahabari wakatapokuwa na uelewa wa masuala mbalimbali yahusuyo TBS itasaidia
kurahisisha kufikisha elimu kwa jamii namna bora ya masuala ya viwango.
Akizungumza wakati akifungua Mkutano huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu
wa TBS,Kaimu Mkurugenzi Mkuu Viola Masako amesema kuifahamu elimu ya viwango
ina faida mbalimbali ikiwemo kuipa serikali urahisi wa kuunga sheria
zinazohusiana na masuala ya afya,usalama na uhifadhi wa mazingira.
Akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa ushiriki katika mchakato wa
uandaaji viwango,Meneja wa Viwango Yona Afrika amefafanua kuwa kiwango
kinapokuwa cha kitaifa utekelezaji wake ni mwananchi yeyote huku akizitaja
faida za viwango kuwa ni pamoja na urahisishaji wa biashara.
‘Faida nyingine za viwango hulinda afya na usalama wa walaji/watumiaji
wa bidhaa mbalimbali lakini pia huondoa mkanganyiko kuhusiana na bidhaa’amesema
Yona
Kwa upande wake Mnja wa Upimaji TBS Joseph Makene akiwasilisha mada
kuhusu huduma zitolewazo na kurugenzi ya upimaji na ugezi amesema vifaa
vinavyotumika katika maabara zilizopo katika Shirika hilo ni vya kisasa na
vinatumia teknolojia ya kisasa.
Hata hivyo imeelezwa kuwa TBS pia hutoa huduma ya kuratibu na
kuthibitisha ubora wa biadhaa kwa kutumia viwango vya kampuni,vya kigeni au vya
kimataifa vilivyothibitishwa na kamati maalum hususani pale ambapo hakujawa na
kiwango cha kimataifa cha bidhaa husika.




Post a Comment