SERIKALI YA TANZANIA YATOA MSIMAMO KUHUSU VITA VYA RUSIA NA UKRAINE
Serikali ya Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu sababu ya kupiga kura ya kutofungamana na upande wowote katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Russia na Ukraine, huku ikisisitiza pande zote mbili kutafuta suluhu katika meza ya mazungumzo.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amesema Sera ya Tanzania kuhusu namna ya kutatua migogoro inapojitokeza ni kwa kutumia njia za kidiplomasia.
Post a Comment