RAIS SAMIA AZINDUA NYUMBA 644 MAGOMENI ,ASISITIZA MIRADI YOTE ITAKAMILIKA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua mradi wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Majengo Tanzania TBA katika eneo la Magomeni Kota Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua mradi wa Nyumba 644 zilizojengwa na Serikali kupitia Wakala wa Majengo Tanzania TBA katika eneo la Magomeni Kota Mkoani Dar es Salaam leo tarehe 23 Machi, 2022.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la wakazi wa Magomeni Kota kuuziwa nyumba kwa utaratibu wa mpangaji mnunuzi, akiwataka waliokuwa tayari kuanza sasa mchakato huo.
Rais Samia ameeleza hayo leo Jumatano Machi 23, 2022 wakati akizindua nyumba hizo zilizojengwa kwa Shilingi 51 bilioni na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mchakato wa ujenzi huo ulianza 2016 na kukamilika mwaka huu.
Katika uzinduzi huo, Rais Samia amefafanua kuwa wakazi hao watatakiwa kurejesha gharama za ujenzi pekee na hawatozwa gharama ya ardhi ili wapate nafuu za kuzinunua.
“Kwa wale wanaotaka kulipa polepole, wanaweza wakaanza sasa mchakato huo ili ikifika miaka mitano, kama umemaliza au unaendelea kulipa na kubaki katika nyumba. Mnaweza kuanza kulipa sasa na mkianza wote kwa pamoja itakuwa vizuri zaidi, niwaombe muanze kulipa sasa,”amesema.
Amesema nyumba hizo ni ahadi ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Magufuli, hivyo atakuwa mstari wa mbele kuendeleza miradi ya watangulizi wake na kutekeleza miradi mipya iliyoahidiwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Post a Comment