Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amekubali kukutana na Putin
Hatimae Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amekubali kwamba Nchi yake haitojiunga na NATO, amemuomba Putin wakae meza moja wamalize tofauti zao.
Jamaa ameendelea kulia na kusikitika kwa kusema sasa imetosha kwani hayupo tayari kuona raia wake wakiendelea kukimbia nchi yao na ameomba Russia wasitishe kupiga mabomu ambayo yanaharibu nchi yao.
Amesema amezidi kuzishangaa nchi za Ulaya pamoja na Majeshi ya NATO kwa kushindwa kumpa msaada wa kijeshi hivyo haoni maana ya kuendelea na msimamo wa kujiunga nao.
Sipo tayari kupiga goti kuomba msaada kutoka NATO, nimewaomba sana msaada lakini hawataki i.e kwa sasa nawapa lawama NATO kwa kushindwa kutoa msaada katika kuokoa vifo na uharibifu wa Ukraine.
"Niko tayari kukutana na Putin kwa mtindo wowote ule ili mradi tuzungumze na kumaliza vita hii" Aliongeza kwa kusema makubaliano yoyote yatakayofanyika lazima yawekwe kwenye kumbukumbu kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Amesema hata kama nchi yake haitojiunga na NATO lakini wao kama nchi hawapo tayari kujisalimisha kwa kushindwa kivita, wanachohitaji ni kuvimaliza hivi vita wakikaa mezani na kukubali ajenda ya kutojiunga na NATO.
Ukraine alitaka kujiunga na NATO ili apate security guarantee kutoka Umoja wa Ulaya na Jeshi lake la NATO, Russia hakutaka Ukraine kujiunga na NATO kwasababu za kiusalama na kujitanua kwa Jeshi la NATO.
Post a Comment