Ads

RAIS SAMIA AFUNGUA RASMI DARAJA LA TANZANITE ,ATOA UJUMBE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kabla ya kufungua rasmi Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach, katika hafla iliyofanyika eneo la Agha Khan Jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoa kitambaa pamoja na Balozi wa Korea hapa nchini Kim Sun Pyo kuashiria ufunguzi rasmi wa Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila pamoja na viongozi wengine wa Serikali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi Rasmi wa Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa wakitembelea na kukagua Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam mara baada ya kulizindua rasmi leo tarehe 24 Machi 2022.



Rais Samia Suluhu Hassan amesema uzinduzi wa mradi wa daraja la Tanzanite ni sehemu ya kumuenzi Rais wa awamu ya tano, John Magufuli.

Ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 24, 2022 Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa daraja hilo lilogharimu Sh243 bilioni.

Rais Samia amesema Desemba 20/2018 aliyekuwa Rais Hayati Magufuli aliweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi huo na kueleza kwamba ni siku ya furaha kuona kazi aliyoianzisha imekamilika.

“Na tumekusanyika hapa kwa ajili ya uzinduzi na kama nilivyosema mara kwa mara kwamba tutakamilisha kazi zote alizozianzisha kwahiyo kwangu mimi uzinduzi wa daraja hili ni sehemu ya kumuenzi Rais John Magufuli,”amesema

Rais Samia amesema serikali ya Korea Kusini ni mdau mkubwa wa maendeleo ambaye amekuwa akiwaunga mkono katika sekta mbalimbali za kimaendeleo hususan kwenye miundombinu.

“Kwaniaba ya wananchi wa Tanzania napenda kutoa shukrani kwa Jamhuri ya Korea ya Kusini kwa mchango wao mkubwa wa maendeleo katika Taifa letu,”amesema

Amesema ujenzi wa daraja hilo ni muendelezo wa Serikali katika kufanya maboresho kwenye sekta ya miundombinu ili kukabiliana na kero ya msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. 

No comments